Ashrack Miraji Same kilimanjaro

Wakazi wa kata ya Hedaru na Makanya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kuondoka kwa muda katika maeneo ambayo si salama hasa walio kwenye mikondo ya Maji yanayotoka milimani .

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni alipofanya ziara katika kata hizo December 7 mwaka huu kwenye kata ya hedaru ambayo November 24 mwaka huu 2023 ilikumbwa na mafuriko yaliyosababisha uharibifu wa Miundombinu ya barabara kuu inayoelekea mikoa ya kazikazini, kubomoa nyumba na kusombwa kwa vyakula , Mifugo na vitu mbali mbali hivyo kuleta hasara kubwa kwa wananchi .

Amesema wananchi ambao wamajenga nyumba zao kwenye mikondo ya Maji waanze kuchukua tahadhari ya kuondoka ili kuepusha madhara makubwa, kuendelea kung’ang’ania kukaa maeneo hayo ni kuhatarisha usalama wao.

“Mtakumbuka yale magogo, mawe na matope yaliyoshuka ule usiku baada ya mvua kunyesha huko mlimani , hali ilikuwa mbaya siku ile naomba tusiwe wabishi tuchukue hatadhari ndugu zangu".Alisema mkuu huyo wa Wilaya.

Ametaka pia jamii Kulinda Wazee na watoto ambao kwa asilimia kubwa muda mwingi hubaki Nyumbani wakati wenye kaya wakienda kujitafutia Kipato kama hakuna Usalama basi wawe wanawaondoka maeneo hayo na kuwaacha maeneo salama zaidi kuepusha madhara inapotokea Mvua kubwa ama mafuriko.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wilaya ya Same jografia yake ni milima mirefu na kumekuwa na historia ya miamba ya milima hiyo kuporomoka kwenye baadhi ya maeneo na kuleta madhara hasa inapofika msimu wa Mvua ikisisitizwa maeneo yaliyo ainishwa na kamati za maafa kuwa ni hatarishi wananchi wachukue hatua za kujihami kwa hiari.

Aidha wananchi wametakiwa pia kujitahidi kuhifadhi vyakula angalau chakula cha zaidi ya miezi miwili kwa tahadhari kwani wilaya ya same ni miongoni mwa wilaya zilizo kwenye mikoa 14 nchini ambazo mamlaka ya Hali ya Hewa wameshaeleza kuwa kutakuwa na mvua zitakazozidi kiwango.

 Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya tayari wamekwisha andika barua kwa mamlaka husika ili tupate wataalam wa miamba ambao watakuja kufanya tadhimini ya miamba ya milima iliyoko wilayani humo ili kujua uimara wake na hatua staki zichukuliwe mapema na serikali.



 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: