Articles by "SAME"
Showing posts with label SAME. Show all posts

 


Na Ashrack Miraji Msumba News

Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, ametoa wito kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, wakiwemo Afisa Ardhi, Mwanasheria na Madiwani, kushirikiana kwa karibu katika kutatua migogoro ya ardhi kwenye kata zote za wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wilayani Same, Mhe. Kasilda alisema Serikali imeweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha migogoro ya ardhi inatatuliwa kwa haraka ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji bila vikwazo.

“Watendaji wote wa Halmashauri, akiwemo Afisa Ardhi, Wanasheria na watendaji waliopo kwenye kata, wanapaswa kushirikiana na Madiwani kufika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazohusiana na ardhi. Haya ni maelekezo mahsusi kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohammed Mchengerwa,” alisema DC Kasilda.

Aidha, aliwapongeza madiwani kwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji, hatua aliyoeleza kuwa inaongeza kasi ya maendeleo katika wilaya.

Katika kikao hicho, Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Same limeidhinisha kwa kauli moja kupandisha madaraja watumishi 230 wa kada mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo. Uamuzi huo umetajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kuongeza morali na ufanisi kazini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Yusto Mapande, alisema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha haki na stahiki za watumishi zinalindwa kwa kuzingatia uwajibikaji na utendaji wa mtu mmoja mmoja.

“Tumekuwa tukipima utendaji wa kila mtumishi kwa kuzingatia vigezo halali. Watumishi waliopandishwa madaraja wamekidhi masharti hayo, na tutaendelea kuhakikisha tunatoa motisha kwa wanaojituma kwa bidii kazini,” alisema Mapande.

Ameongeza kuwa Halmashauri itaendelea kufanya tathmini ya mara kwa mara kwa watumishi wake ili kuhakikisha ufanisi unabaki kuwa kigezo kikuu cha maendeleo ya taasisi hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa maadili na nidhamu kazini.





 

Na Ashrack Miraji –

Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, ameonyesha kutoridhishwa na usimamizi wa mradi wa maji unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Kata ya Kisiwani. Licha ya serikali kutoa shilingi milioni 720 kwa ajili ya mradi huo, bado haujanufaisha walengwa, huku baadhi ya wananchi wakidaiwa kujiunganishia maji kinyemela.

Hali hiyo ilibainika katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Kisiwani Barazani, ambapo msimamizi wa mradi alishindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu gharama za mradi, idadi ya walengwa, na hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliojiunganishia maji kinyemela. Kukosa kwake majibu kulizua maswali mengi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, wataalamu, na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Mhe. Kasilda Mgeni alieleza kutoridhishwa na hali hiyo, akisisitiza kuwa ni jambo lisilokubalika kwa msimamizi wa mradi kushindwa kueleza thamani ya fedha zilizotolewa, watu waliopaswa kunufaika, na maendeleo ya mradi.

“Yaani kimsingi umenichefua! Kama hii kazi huitaki, sema, kuna watu wanashida na hizi kazi. Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta milioni 720 hapa, na RUWASA ndio mmepewa jukumu la kuutekeleza. Thamani ya hela mliyoletewa hujui, ulilenga kunufaisha watu wangapi hujui! Hapa lazima hatua kali zichukuliwe. Haiwezekani watu wanapewa mradi mkubwa wa milioni 720, halafu mwisho wa siku maji hayatoki, wala hawajali! Hawajui wananchi wangapi wanapaswa kuhudumiwa na huo mradi, hawajui!” alisema kwa hasira.

Aidha, Mhe. Mgeni aliwataka wananchi wote waliounganisha maji kinyemela kujisalimisha mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Pia, aliwaagiza wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata kufuatilia na kuwabaini wote waliohusika katika vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua stahiki.

“Waliojiunganishia maji, niwaombe mjisalimishe kabla hamjakamatwa. Ninyi mnafanya wenzenu wakose maji. Ninyi ni wezi kama wezi wengine wanaoiba mali za umma. Hii ni haki ya wananchi wote, si ya wachache wanaochukua kwa ujanja. Hatutavumilia hali hii, na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika,” alisisitiza.

Mkuu wa Wilaya ameagiza RUWASA kutoa maelezo ya kina kuhusu matumizi ya fedha za mradi, idadi ya walengwa, na hatua zitakazochukuliwa ili kuhakikisha maji yanawafikia wananchi waliokusudiwa.

Mradi huo wa maji katika Kata ya Kisiwani ulilenga kunufaisha jumla ya wananchi 3,150, huku gharama halisi ya utekelezaji wake ikiwa shilingi milioni 722.2. Hata hivyo, mradi huo umeshindwa kufanikisha malengo yake kutokana na changamoto za usimamizi, jambo ambalo sasa linahitaji hatua madhubuti za ufuatiliaji na uwajibikaji.    

Ashrack Miraji Same kilimanjaro

Wakazi wa kata ya Hedaru na Makanya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kuondoka kwa muda katika maeneo ambayo si salama hasa walio kwenye mikondo ya Maji yanayotoka milimani .

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni alipofanya ziara katika kata hizo December 7 mwaka huu kwenye kata ya hedaru ambayo November 24 mwaka huu 2023 ilikumbwa na mafuriko yaliyosababisha uharibifu wa Miundombinu ya barabara kuu inayoelekea mikoa ya kazikazini, kubomoa nyumba na kusombwa kwa vyakula , Mifugo na vitu mbali mbali hivyo kuleta hasara kubwa kwa wananchi .

Amesema wananchi ambao wamajenga nyumba zao kwenye mikondo ya Maji waanze kuchukua tahadhari ya kuondoka ili kuepusha madhara makubwa, kuendelea kung’ang’ania kukaa maeneo hayo ni kuhatarisha usalama wao.

“Mtakumbuka yale magogo, mawe na matope yaliyoshuka ule usiku baada ya mvua kunyesha huko mlimani , hali ilikuwa mbaya siku ile naomba tusiwe wabishi tuchukue hatadhari ndugu zangu".Alisema mkuu huyo wa Wilaya.

Ametaka pia jamii Kulinda Wazee na watoto ambao kwa asilimia kubwa muda mwingi hubaki Nyumbani wakati wenye kaya wakienda kujitafutia Kipato kama hakuna Usalama basi wawe wanawaondoka maeneo hayo na kuwaacha maeneo salama zaidi kuepusha madhara inapotokea Mvua kubwa ama mafuriko.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wilaya ya Same jografia yake ni milima mirefu na kumekuwa na historia ya miamba ya milima hiyo kuporomoka kwenye baadhi ya maeneo na kuleta madhara hasa inapofika msimu wa Mvua ikisisitizwa maeneo yaliyo ainishwa na kamati za maafa kuwa ni hatarishi wananchi wachukue hatua za kujihami kwa hiari.

Aidha wananchi wametakiwa pia kujitahidi kuhifadhi vyakula angalau chakula cha zaidi ya miezi miwili kwa tahadhari kwani wilaya ya same ni miongoni mwa wilaya zilizo kwenye mikoa 14 nchini ambazo mamlaka ya Hali ya Hewa wameshaeleza kuwa kutakuwa na mvua zitakazozidi kiwango.

 Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya tayari wamekwisha andika barua kwa mamlaka husika ili tupate wataalam wa miamba ambao watakuja kufanya tadhimini ya miamba ya milima iliyoko wilayani humo ili kujua uimara wake na hatua staki zichukuliwe mapema na serikali.



 

Ashrack Miraji ; Same kilimanjaro

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha  mapinduzi CCM Wilaya ya SAME Cde.Azza Karisha amehitimisha mashindano ya SAMIA CUP yaliyokuwa yanachezwa kwenye Tarafa ya Mamba Vunta, Jimbo la Same Mashariki michezo iliyo andaliwa na Mbunge wa Jimbo Hilo mhe.Anne Kilango.

Mashindano hayo yamehitimishwa kwa mchezo wa  Fainali uliokutanisha timu za Nyuki FC kutoka Kata ya Vunta na  Zimbwe FC kutoka kata ya Mpinji amapo timu ya Zimbwe FC iliibuka mshindi kwenye fainali hiyo na kutangazwa kuwa Mabingwa wapya.

Pamoja na mambo Mengine Mwenyekiti huyo wa UVCCM amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango  kwa kuamua Kuanzisha Mashindano ikiwa ni Sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM akisema Mashindano hayo yamekuwa na tija kubwa kwa Vijana kwa maana ya Kujenga umoja, Upendo, mshikamano  Lakini pia na kuimarisha afya zao.

"Niendelee  Kumshukuru na Kumpongeza Mwenyekiti wetu was chama Taifa ambae ndie Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani na serikali yake kwa namna ambavyo amewajali Wananchi wa Tarafa ya Mamba Vunta na Kuwaletea Fedha Nyingi za Maendeleo kwenye sekta Mbalimbali ikiwepo Elimu, afya, barabara, kilimo nk". Alisema Mwenyekiti huyo wa UVCCM wiaya ya Same.

Pamoja na hayo amewaomba  wananchi wa Mamba Vunta kuendelea kumuunga Mkono Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani na  Mbuge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango na chama Cha Mapinduzi kwani ndicho akisema ndio  chama pekee kinachoweza Kuwaletea Wananchi Maendeleo.

Aidha  katika hatua nyingine mwenyekiti huyo aliongoza zoezi la upandaji Miti kwenye shule ya  Msingi Mpinji mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya Utunzaji wa Mazingira na kuifanya Same iwe ya kijani.

Katibu wa Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Semu Mmamba Amesema jimbo la Same Mashariki lina tarafa tatu tarafa Moja wamemaliza mashindano hayo bado tarafa mbili kila tarafa inapaswa kutoa mshindi wa kwanza mpaka watatu hili kupata Timu 9 ambazo zitaunda Tena mashindo ya Samia Cup washindi wa tatu wanaopatikana kwa kila tarafa watapatiwa zawadi baada ya mashindano hayo kukamilika  na kumpata mshindi wa jimbo wa ligi ya SAMIA CUP.