1000412340


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema wananchi 2,400 wanaopisha mradi wa uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi wataanza kulipwa fidia kuanzia kesho.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wanaoathiriwa na uendelezaji wa Bonde hilo kwenye eneo la Jangwani jijini Dar es salaaam.

Amesema fidia hiyo inalipwa kwa wananchi wote waliokubali kulipwa na kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao za kibenki ili kupisha utekelezaji wa mradi huo na tayari Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha kwa ajili hiyo.

"Nimekuja leo kutoa tamko ya hatua ya uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi uanze mara moja kuanzia sasa na hii iende sambamba na ulipaji wa fidia kutokana na tathmini iliyofanywa na wataalam, natambua kabisa wapo wananchi asilimia 92 kati ya wote wanatakiwa kulipwa fidia wanasubiria fedha zao na sikatai wapo wengine wenye malalamiko wataalam wangu endeleeni kuyafanyia kazi na mkishindwa yaje kwangu nione hatua ya kuchukua,"amesema.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema hapa Katika Misingi ya ukaaji kwenye maeneo wa hatarishi Sheria inaondoa ulipaji wa fidia kwa wakazji wa maeneo hayo lakini Mkuu wa Mkoa na Mhe. Diwani wamewaombea na kusema hili haliwezekani wananchi wetu tunaomba walipwe hata kifuta Jasho namimi nikazungumza na Mhe. Rais na akaridhia kila mmoja alipwe kifuta Jasho cha Sh. Milioni nne,"amesema.

1000412341

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Albert Chalamila amesema kwa wale wenye malalamiko atawasikiliza na litakalohitaji kupelekwa kwa Mhe. Waziri atalipeleka.

Naye, Mratibu anayesimamia Miradi inayotekelezwa na Benki ya Dunia, Mhandisi Hamphrey Kanyeye amesema wananchi wa Mitaa 16 watalipwa malipo mbalimbali kutokana na thamani ya vitu walivyonavyo.

"Malipo hayo yatajumuisha kifuta jasho, usumbufu, mali pamoja na kodi ya nyumba ya miaka mitatu kwa wale wananchi waliokuwa na nyumba eneo hilo na wanaishi ili wapate fedha za kulipia kodi ya nyumba kipindi wanaendelea na ujenzi,"amesema.

Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza mradi huo unaolenga kukabiliana na mafuriko na kuboresha matumizi ya ardhi katika eneo la chini la Bonde kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB) wa takribani Sh. Bilioni 598 na Sh.Bilioni 600 nyingine zimetolewa na Hispania na Uholanzi.
1000412346
1000412342
1000412343
1000412344
1000412345
Share To:

Post A Comment: