Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa wataalamu wa Akili Bandia , ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 15,2023 jijini Arusha.



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Professa Lughano Kusiluka akitoa salamu kwa wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa wataalamu wa Akili Bandia ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 15,2023 jijini Arusha.



Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Maulilio Kipanyula akitoa salamu kwa wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa wataalamu wa Akili Bandia ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi hiyo Novemba 15,2023 jijini Arusha.

  

Wataalamu wa Akili Bandia wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa kwanza wa kimataifa uliofanyika Novemba 15,2023 jijini Arusha .

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Omary Kipanga akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Akili Bandia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa wataalamu hao Novemba 15,2023 jijini Arusha.



Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeleza kuwa imeshandaa Sera ya masuala ya Akili Bandia ambayo inatoa muongozo wa namna ya kusimamia teknolojia hiyo inayokuwa kwa kasi duniani.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga wakati akifungua mkutano wa kwanza wa kimataifa wa wataalamu wa Akili Bandia ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 15,2023 jijini Arusha.

"Kama Taifa tupo tayari katika kutumia teknolojia hii ya akili bandia katika masuala ya tehama ili kuhakikisha matumizi ya teknolojia zinazokuwa kwa kasi zinatumiwa ipasavyo" amesema Mhe. kipanga.

Ameeleza kuwa, mapinduzi ya nne na ya tano ya viwanda yanapelekea kutegemea kutumia kwa kiasi kikubwa akili bandia kuliko mikono ya binadamu, na Serikali ina wajibu wa kutengeneza miundo mbinu bora katika kuhakikisha utekelezaji wake.

Mhe. Kipanga amesema akili bandia haijaondoa uhalisia wa akili za binadamu hivyo hayataharibu mfumo wa elimu bali utazidi kuimarika zaidi, huku akisisitiza kuwa vyuo vikuu vinatayarisha vijana kwa ajili ya kushiriki katika kuleta maendeleo zaidi.

Wakati huo huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Professa Lughano Kusiluka ameeleza kuwa, akili bandia ni sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) endapo wasomi wa vyuo vikuu watatumia akili bandia katika maandiko yao, watapata kazi kubwa ya kuelezea uhalisia mbele ya jopo la walimu mahiri wanaowasimamia.

" Vyuo vikuu vipo macho kuangalia ujio wa teknolojia hii na endapo wasomi watabainika kutumia akili bandia kwa kiasi kikubwa kuliko uhalisia tutawafukuza vyuoni wala hatutaki mchezo" Prof. Kusiluka

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya NelsonMandela(NM-AIST) Profesa Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, taasisi nyingi zinatumia akili bandia hivyo ni lazima kujengewa uwezo katika tehama kuhakikisha tafiti mbalimbali zinazofanyika zinaendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika kuleta maendeleo kwa wananchi juu ya changamoto zinazoikabili jamii.
Share To:

Post A Comment: