Na Moreen Rojas, Dodoma.


Bodi ya mkonge Tanzania imeanza zoezi la kukodisha mashamba kwa wakulima wadogo kwa elfu 11 kwa ekari mwaka mzima ili kuwasaidia wakulima ambapo 

ongezeko kubwa la wakulima wadogo, hadi mwaka 2020 TSB iliweza kusajili wakulima wadogo 6887. Mwaka 2022 idadi ya wakulima wadogo waliosajiliwa ni 8972.


Hayo yameelezwa na Saddy Kambona Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) wakati akuzungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kueleza utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2023/24.



 Hata hivyo wakulima wadogo wa Mkonge ambao hawajafikiwa na kusajiliwa na TSB wanakadiriwa kufikia 22,000 kutokana na hamasa kubwa ya kilimo cha Mkonge iliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo, OR-TAMISEMI kupitia Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Bunge na Bodi ya Mkonge Tanzania.


"Kuongezeka kwa mashamba ya kulima Mkonge hasa kwa wakulima wadogo ambapo TSB imegawa mashamba kwa wakulima 983 Wilayani Korogwe na wakulima wengine zaidi ya 3000 wamegawiwa mashamba Wilayani Kilosa na zoezi bado linaendelea,hii ni baada ya Mheshimiwa Rais kufuta mashamba pori Wilayani Kilosa, Morogoro na kuiongezea mashamba TSB kwa ajili ya kuwagawia wakulima wadogo walio tayari kulima mkonge pamoja na kushusha riba kwenye mabenki ya biashara kwa mikopo inayoelekezwa kwenye kilimo na hivyo kuleta unafuu mkubwa sana kwa wakulima,riba kwa mikopo ya kilimo sasa kwa ujumla haizidi asilimia 9%." Amesisitiza Kambona



Aidha bodi imefanikiwa kununua mitambo mipya ya kuchakata Mkonge (Korona) na kufufua mitambo ya kuchakata Mkonge ya Mashamba ya Kibaranga Wilayani Muheza, Tanga na shamba la Serikali la TPL lililopo Kata ya Bwawani Wilayani Arumeru, Arusha ambalo linasimamiwa na kuendeshwa na TSB,mitambo hii itasaidia sana kuongeza uzalishaji wa Mkonge na hivyo kuwezesha kufikiwa kwa lengo la uzalishaji lililowekwa na Serikali,hii inaonesha kwamba Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuimarisha kilimo na kuhakikisha kuwa kilimo kinakua kufikia asilimia 10 ifikapo Mwaka 2030 (Agenda 10/30 kilimo ni biashara.


Aidha kuanzia mwaka 2018, Serikali iliamua kuchukua hatua za makusudi za kufufua zao la Mkonge na kuifufua na kuijenga upya Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB). Mwaka 2019 Serikali ililiingiza zao la mkonge katika orodha ya mazao ya kimkakati na kufanya zao hilo kuwa zao la saba la kimkakati,mazao mengine ya kimkakati ni Pamba, Tumbaku, Kahawa, Korosho, Chai, Michikichi,zao la Mkonge likaingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 ambamo limewekwa lengo la kuongeza uzalishaji kutoka tani 36,000 zilizokuwa zinazalishwa kwa Mwaka 2020 hadi kufikia tani 80,000 kwa Mwaka, ifikapo Mwaka 2025.


"Serikali ikaongeza lengo na kuiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania kuhakikisha kuwa uzalishaji unaongezeka hadi kufikia tani 120,000 kwa mwaka, ifikapo mwaka 2025/2026,hatua za Serikali kuliingiza zao la mkonge kwenye orodha ya mazao ya kimkakati ilitokana na ukweli kwamba mahitaji na soko la mkonge limezidi kuimarika duniani,hii ni kutokana kugundulika kwa matumizi mapya ya mkonge na uzalishaji wa bidhaa mpya zitokanazo na mkonge kama vile vifaa vya ujenzi(gypsum boards, Matofali,mbao, mabati, vigae), Sukari ya Mkonge, Pombe ya Mkonge, Karatasi maalum, Bio Gas, mbolea, Chakula cha mifugo , urembo, mabodi ya magari n.k."Amesema Kambona


Mkonge ulikuwa unalimwa na wakulima wakubwa pekee waliokuwa wanamiliki mashamba makubwa (Estates/Plantations), hakukuwa na wakulima wadogo wa mkonge, uzalishaji wa mkonge uliongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia mwaka 1964 Tanzania iliweza kuzalisha takriban Tani 230,000 na kuongoza Duniani kwa uzalishaji wa zao la mkonge,kipindi hicho Mkonge ulikuwa unachangia takriban 65% ya fedha za kigeni nchini kabla ya uzalishaji kuanza kuporomoka kuanzia mwaka 1970 ambapo hadi kufikia Mwaka 1997 uzalishaji wa Mkonge kwa Mwaka ulikuwa ni tani 19,000 tu.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: