Mashabiki   wa Timu za Simba na Yanga ambao ni watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru(TICD), wamecheza mechi ya kirafiki katika juhudi za kuendelea kudumisha mahusiano na ushirikiano katika maeneo ya kazi.

Akizungumza katika bonanza hilo Mgeni rasmi Kaimu Naibu Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD),anayeshughulikia Mipango na Utawala bi.Janeth Zemba  alisema kuwa lengo hasa la bonanza hilo ni kuendelea kutangaza taasisi hiyo kupitia michezo.

"Bonanza hili ni la tatu kufanyika na leo hakuna aliyepatikana mshindi kwa kuwa sio mashabiki ya Simba wala Yanga aliyemfunga  mwenzake hivyo tutaendelea kushirikiana katika  michezo kwa kuwa inajenga mahusiano mema,ni furaha amani na pia inatuweka vizuri kiafya kupitia mazoezi tunayoyafanya mwaka mzima hivyo  tutaendelea kuboresha na kushirikiana  pia na wadau mbali mbali ".Alisema bi.Zemba

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaasa wadau mbali mbali kuendelea kudumisha mshikamo na ushirikiano,na kuendelea kuitangaza taasisi hiyo kupitia sekta hiyo ya burudani ambayo inaleta makada mbali mbali.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Daktari Bakari George alisema kuwa bonanza hilo  linaleta watumishi na jamii ya maendeleo ya tengeru pamoja na ni mfulululizo wa bonanza ambalo linawakutuanisha pia na watu maarufu ambao wamewahi kutumikia vilabu vikubwa nchini vya Simba na Yanga.

"Mwaka Jana katika bonanza kama hili tuliwashirikisha wasemaji wa timu hizi mbili na Leo pia Mwaka huu tuna wachezaji ambao ni Mrisho Khalifan Ngassa ambaye amewahi kucheza katika klabu ya Yanga na Daniel Mrwanda ambaye aliwahi kucheza katika timu ya Wekendu wa Msimbazi Simba na timu ya Taifa pia "Alisema dkt.Bakari 

Dkt.Bakari alisema kuwa nia kubwa ni hamasa ya michezo na vilevile kuitangaza taaisisi hiyo ya TICD,kupitia sekta ya michezo ambayo huleta watu wengi pamoja.

Hata hivyo alisema kuwa bonanza hilo ni kichocheo kikubwa kwa watumishi kuendelea kufanya mazoezi mwaka mzima na kulete tija katika maeneo ya kazi.

Bonanza hilo limekutanisha mashabiki wa timu ya Simba na Yanga kutoka katika viunga wa mkoa wa Arusha,ambapo limekuwa likijipatia umaarufu mwaka hadi mwaka ambapo lengo ni kulipeleka katika maeneo mengine nchini.

Mechi ya utangulizi ilikutanisha timu ya Wanafunzi wa chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga,ambapo matokeo yalikuwa ni 1-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa chuo Cha Mifugo Tengeru.













Share To:

Post A Comment: