Wananchi wanaoishi Kata ya Nduruma katika halmashauri ya Arusha DC wameondokana na kero ya ubovu wa barabra ambapo  Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) wameanza kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo ya Malalua -Nduruma yenye urefu wa kilomita 28 ikiwa na thamani ya sh, bilioni 30.8 itakayowaondolea kero ya usafiri ikiwemo usafirishaji wa mazao yao. 

Shukrani hizo zilitolewa na wananchi hao mara baada ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Asmil Ali Ussi wakati mwenge huo ulipoweka  jiwe la msingi na kukaguliwa barabara hiyo. 

Elizabeth Kaaya alisema awali barabara hiyo ya ilikuwa na changamoto sababu ya mashimo na vumbi linaloleta kero kwa wasafiri hali iliyopelekea daladala kupandisha nauli kutoka sh,2500-3000 badala ya sh, 1500.

Alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutasaidia maendeleo kupatikalisema ambio za mwenge ameagua mradi wa uboreshaji wa barabara kwa ni awali

 Ilikuwa na changamoto kubwa kwa wananchi hao huku  dereva wa bodaboda Lazaro Marko mkazi wa kitongoji cha bwawani akiishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo awali ilikuwa na changamoto

"Sisi wananchi tunaishukuru serikali kwa kutengeneza barabara hii ya Nduruma awali ilikuwa ni kero lakini pia kwa bodaboda napo bei juu kuliko mahali unapoenda, tunaomba barabara hii ikamilike kwa wakati kwani leo wamezindua ujenzi wa mita 600

Ambapo Mkimbiza mwenge,Usi alisisitiza barabara hiyo kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kuitumia kusafirisha bidhaa zao na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto za wananchi hususan katika sekta ya miundombinu ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa

Awali Meneja wa Tarura Wilaya ya Arumeru, Injinia Julius Kaaya alisema barabara hiyo ilianza kujengwa Septemba 13,2024 na inatarajia kumalizika Agosti 8,2025



Share To:

Post A Comment: