Mwenge wa UhuruWanafunzi wa zaidi 80 wanaosoma shule ya sekondari Malula kata ya Malula Wilayani Arumeru wameondokana na adha ya mabweni baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)kujenga bweni lenye thamani ya milioni 168.4
Uzunduzi wa bweni hilo ulifanywa na Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Ismail AliUssi mara baada ya kukagua bweni hilo lenye vyumba 20 vitanda 40 na kupongeza juhudi za serikali katika kuinua sekta ya elimu
Alisema mradi huo ni wa kimkakati unaopelekea wanafunzi kupata elimu bora , ndio maana serikali imeboresha sekta ya miundombinu ya elimu ili kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unaongezeka zaidi.
"Mradi huu umetekelezwa kwa ufasaha chini ya Uongozi wa Rais Samia Hassan Suluhu hivyo alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mwinyi Ahmed Mwinyi na viongozi wengine kwa ujenzi wa shule hiyo katika kuhakikisha kiwango cha elimu kinaongezeka"
Alisisitiza wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu hivyo na kuwapongeza wanafunzi kupitia klabu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) kuhakikisha wanatekeleza uadilifu na kushika yale yote wanayoelekezwa ili kupinga rushwa ikiwemo walimu kusimamia wanafunzi hao kupata elimu na kuendelea na mapambano dhidi ya rushwa
Akisoma taarifa ya mradi huo Mwenyekiti wa Kamati inayosimamia miradi ya Tasaf, Onesmo Nanyaro alisema mradi huo utasaidia wanafunzi kusoma kwa bidii ikiwemo kuondokana na adha ya ukosefu wa malazi
Awali akipokea mwenge wa uhuru kutoka Mkoani Kilimanjaro , Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Kihongosi alisema mwenge huo utazindua miradi 54 yenye thamani ya sh, bilioni 30.3 katika halmashauri saba
Mwenge huo uliwasili jana mkoani Arusha na kukabithiwa eneo la King'ori Kibaoni Wilayani Arumeru ukitokea Mkoani Kilimanjaro ambapo utapitia miradi 54 kisekta yenye thamani ya sh, bilioni 30.3 mkoani hapa.
Post A Comment: