Na Moreen Rojas, Dodoma. 

Kufuatia Asali ya Tanzania kufanya Vizuri katika masoko ya kimataifa Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Dos Santos Silayo ametoa rai kwa watanzania kuongeza wigo wa uzalishaji wa mazao ya nyuki yaliyoongezwa thamani.


Moja ya mazao ya misutu ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo ni zao la Asali ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozalisha Asali bora duniani kwa asilimia 96.


Profesa Dos Santos Silayo ni Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania amezungumza hayo leo Jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari akisema kwa mujibu wa shirika la chakula Duniani Tanzania inakadiriwa kuwa na makundi ya nyuki (bee colons) takribani milioni 9.2 huku Uzalishaji wa mazao ya nyuki ukiongezeka.


Profesa Silayo amesema Wakala unasimamia hifadhi za nyuki 20 zenye ukubwa wa hekta 39,444 huku  Uzalishaji wa mazao ya nyuki ukiongezeka na kuzalisha wastani wa tani elfu 33 zikizalishwa kwa mwaka.


"Tutajitahidi tuhakikishe vijana wengi wanaingia kwenye biashara ya nyuki kwani miradi hii imekuwa ikifanywa na kina mama pekee niwashauri vijana wasisite kujaribu biashara hii kwani watapata faida kubwa"Amesisitiza Prof.Silayo


Aidha amesema kuhusu ukusanyaji wa maduhuli na mchango kwenye mfuko mkuu wa serikali Hadi kufikia Juni, 2023 jumla ya Shilingi Bilioni 143.5 ambayo ni sawa na asilimia 96 ya makisio ya miradi yote zilikusanywa. 


" Katika kipindi cha miaka miwili TFS tumeanzisha shamba jipya moja la Makerere (65,000ha)Kasulu Kigoma na kufanya upanuzi wa mashamba mawili yanayolima Teak(Mtibwa ha12,000 range ya Pagale na Longuza ha 400"Amesema Prof.Silayo


Kutokana na utekelezaji wa Majukumu ya wakala kwa ufanisi, Wakala umetunukiwa tuzo mbalimbali ikiwemo Tuzo ya Mshindi wa pili ya asali ya kimiminika rangi nyeusi iliyotolewa katika Kongamano la Apimondia nchini Afrika Kusini, March 2023. 


Sekta ya Misitu na nyuki nchini ni muhimu kutokana na mchango wake mkubwa katika ukuaji wa sekta nyingine za uzalishaji kama vile utalii, maji, kilimo, mifugo na nishati pamoja na sekta ya viwanda. 


"Kwa kuzingatia uelewa huo Tanzania ina eneo la misitu 48.1 milioni ambapo ni sawa na asilimia 54% ya eneo lote,tathimini hii ni misitu yote bila kujali umiliki au mifumo ya ikologia kwa Tanzania misitu ya ikologia ya miombo ndo inachukua eneo kubwa zaidi ya 93%" Amefafanua Prof.Silayo



Lengo Kuu la kuanzishwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni kuhakikisha uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki, Upatikanaji wa bidhaa za mazao ya misitu na nyuki nchini,Kukusanya maduhuli ya serikali kutoa huduma kwa umma na kuendeleza rasilimali watu .

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: