Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel.
..........................................................
Na Dotto Mwaibale, Arusha
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) unatarajia kuwakutanisha wanamuziki,
wananchi, viongozi na wadau mbalimbali
katika Tamasha kubwa litakalohusu mchango wa wanamuziki katika maendeleo
ya nchi ambalo litafanyika kwa siku tatu jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel
alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwa kwaya mbalimbali na wanamuziki
binafsi watakuwepo kutoa burudani.
"Tamasha hilo litakuwa la siku tatu na litafanyika katika Makumbusho
ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa kuanzia Agosti
25 hadi Agosti 27, 2023," alisema Joel.
Alisema makundi ya kwaya na waimbaji binafsi watakuwepo kutoa burudani
wakiongozwa na kwaya Kuu Habari Njema ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania|KKKT } na Kwaya ya Tangazeni ya kanisa hilo Unga Limited zote za
jijini Arusha.
Alisema pia kutakuwa na bendi kutoka mikoa mbalimbali ambazo zitashiriki
kutoa burudani kwenye tamasha hilo kubwa na la aina yake.
Alitaja kundi lingine ambalo litakuwepo ni wadau wa maendeleo ambapo pia
kutakuwepo na fursa mbalimbali na kuwa kiingilio ni bure.
Joel alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wa
muziki kufika kwenye tamasha hilo ambapo aliwataja baadhi ya wadau watakao
kuwepo kuwa ni pamoja na Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi |Dodoma ], Dkt.Noelia Myonga, Agness Kanuty, Mwenyekiti wa Nokongo, Dkt.
Lilian Badi na Mkurugenzi wa Makumbusho
ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha, Dkt. Christina Ngereza.
Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard alisema katika tamasha hilo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na COSOTA na TAMRISO watakuwepo kutoa elimu na usajili wa wanamuziki.
Post A Comment: