Screenshot_20230810-164937%257E3


MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA ) imepanga kutumia Sh Bilioni 8 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu Nchini.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bahati Geuzye ,Leo Agosti 10,2023 Jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.

Amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 mamlaka hiyo imepanga kutumia kiasi cha Sh bilioni nane kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini

Amesema kiasi hicho cha fedha kitatumika kufadhili miradi 82 katika shule 81 zikiwemo shule 48 za msingi na 33 za sekondari katika maeneo mbalimbali Tanzania bara.


Screenshot_20230810-164849

Miradi hiyo itakapokamilika itawanufaisha wanafunzi 39,484 na walimu 169 katika shule za msingi na sekondari.

Geuzye amesema miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 82, matundu ya vyoo 336, mabweni 10,, ujenzi wa maabara 18 za masomo ya sayansi na nyumba za walimu 32.

Pia amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024, TEA itatoa ufadhili kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika taasisi moja ya elimu Tanzania Zanzibar, mradi huo umepangwa kutumia milioni 300 katika utekelezaji wake.

Amesema kuwa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, TEA inafadhili miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika ngazi zote za elimu kwa Tanzania bara na ngazi ya elimu ya juu kwa Tanzania Zanzibar.

Amesema kuwa kupitia Mfuko wa Elimu wa taifa unaoratibiwa na TEA kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Sh bilioni 10.99 ziligharamia ufadhili wa miradi 132 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini, miradi hiyo ilijumuisha ujenzi wa madarasa 114 katika shule 38.

Pia maabara 10 za sayansi katika shule tano za sekondari , matundu ya vyoo 888 katika shule 37 za msingi 29 na sekondari nane , miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na utoaji wa vifaa vya kujifunzia na kujifunzia katika shule nane za msimgi.

Amesema kuwa miundombinu hiyo imehusisha ujenzi wa madarasa 10, matundu vya vyoo 50 na mabweni matatu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Ametaja miradi mingimne iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 ni pamoja na ujenzi wa nyumba 52 za walimu katika shule 13 pamoja na ujenzi wa majengo ya utawala saba katika shule sita za sekondari na moja ya singi, miradi hiyo imenufaisha jumla ya wanafunzi 22,556 na walimu 123 nchini kote.

“TEA ambayo ni miongoni mwa Taasisi wa muungano kupitia Mfuko wa Elimu imetoa ufadhili wa Sh milioni 500kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa miundombinu pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufuindishia na kujifunzia katika vyuoviwili vya elimu ya juu vilivyopo Tanzanua Zanzibar,” amesema

Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa katika ufadhili huoTaasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST) ilipokea ufadhili wa Sh milioni 200na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) kampasi ya Benjamin Mkapa iliyopo Pemba ilipokea ufadhili wa Sh milioni 300, ufadhili huoumenufaisha wanafunzi 700 katika vyuo hivyo viwili.

Amesema kuwa katika kuunga mkono serikali kuhamia Dodoma , TEA kupitia Mfuko wa Elimuilifadhili miradi mikubwa miwili ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya msingi inayofundisha kwa lugha ya kiingereza ya Msangalele kwa thamani ya Sh milioni 750 katika mwaka wa fedha 2021/2022.

Aidha mfuko ulifadhili ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu katika shule nne za msingi za Jijini Dodoma ambazo ni Kisasa, Kizota, Medelin a Mlimwa C kwa thamani ya Sh bilioni 1.9

Mkurigenzi huyo ameongeza kuwa, pamoja na kuratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa, TEA ilipewa jukumu na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia katika mwaka wa fedha 2017/2018 kusimamia Mfuko wa kuendeleaza Ujuzi(SDF).

Amesema kuwa mfukohuo unasimamiwa na Benki ya Dunia pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umekamilisha utekelezaji wake wa miradi katika awamu yakwanza ya ESPJ katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema kuwa jumla ya Sh bilioni 20.1 zimetumikakatika utekelezaji wa miradi katika taasisi 235 chini ya SDF tangu mwaka wa fedha 2018/2019 hadi mwaka 2022/2023.

Pia amesema Serikali imefanikiwa kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kufikia wanufaika 49,053 sawa na asilimia 114 ya wanufaika waliolengwa.

Amesema kuwa program za mafunzoya ujuzi zilizofadhiliwa na SDF zimeweza kuwanufaisha wanawake 22,413 sawa na asilimia 46 na wanaume 26,650 sawa na asilimia 54 ya wanufaika.

Amesema kuwa jumla ya vijana walionufaika ni 464, waliotoka kundi la wenye ulemavu vijana 2,928
Share To:

Post A Comment: