Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Peter Serukamba Ametoa Rai kwa Benki Kuu ya Tanzania kusaidia kikundi cha Waalimu kinachoendelea kukopa fedha kwenye Taasisi ambazo Hazijapewa leseni kutoka Benki Kuu.


Amesema Benki Kuu linajukumu la kutoa kibaumbele kwa Vikundi vya Waalimu na makundi mengine yanayoonekana kukopa fedha katika vikundi hivyo visivyo rasmi.


Mheshimiwa Serukamba ametoa Rai hiyo alipotembelea Banda la Benki kuu katika sherehe za maonesho ya nanenane kanda ya kati katika viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.


“Saidieni Waalimu nchini ambao wanaongoza kukopa Pamoja na kwamba wamesoma ila wanaonewa na hizo Taasisi Makundi mengine mnayoyagundua pia hakikisheni mnafikisha elimu kwa watu wengi zaidi kwani taasisi isiyo rasmi inatuumizia wananchi wetu kwa kutoza riba kubwa.” Amesema Mh.Serukamba 


Awali akizingumza Afisa Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Potamia Mamsey Amesema Benki Kuu inatoa leseni kwa Taasisi zinazokopesha fedha kwa kuzingatia Riba zisizo waumiza wanachi.


Amesema Benki Kuu imekua ikitembelea Taasisi ndogo wanaopatiwa leseni kujiridhisha na utendaji wao wa kazi.


“Kwanza wanaleta Sera zao za Mikopo na katika sera zao wanakua wameidhinisha riba watakazo toza kwa wananchi na Hatutoi Leseni kwa Taasisi zenye kutoa mikopo yenye riba umiza kwa wananchi ”


Na Kuongeza kuwa “Tunapoenda kwenye ukaguzi kama riba wanazotoa zimekua kubwa tunachukulia hatua na kuwaripoti kwahiyo tunatoa hamasa kwa wananchi kuchukua mikopo kwenye Taasisi zilizopowa leseni ya kufanya hizo shughuli na Benki Kuu”.Amefafanua Mamsey



Bi. Mamsey ametoa Rai kwa wananchi kusoma na kuelewa masharti ya Mikataba kabla ya kuchukua mikopo ili kuepusha na kwamba watanzania wengi wamekua waliangalia changamoto zao na kuchukua mikopo kwa kuangalia tatizo alilokua nalo Bila kusoma Vizuri mikataba.


Kumekua na Desturi ya wananchi Kukimbilia mikopo katika Taasisi hizo zisozo rasmi na kuacha kukopa katika Taasisi zilizopewa leseni.


Amesema Benki inafanya hatua kadhaa za kutatua changamoto ya wananchi kukimbilia Taasisi ambazo hazijapewa leseni ikiwa ni Pamoja na kutembelea Taasisi ndogo ndogo ambazo hazijasajiliwa na kuwahamasisha wananchi wanapoenda kukopa wakiona Taasisi hizo hazina leseni waweze kuziripoti Benki Kuu na Benki.


“Titakachokifanya ni kutembelea uongozi wa eneo husika kama anatambua Taasisi hizo na kuzuia Huduma hizo pia tutawapatia elimu huenda hata wao hawajapata elimu ya kupata leseni. ”Amefafanua Bi.Mamsey

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: