Watumishi wa umma nchini karibu watakopeshwa magari ya Serikali ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Hayo yamedhihirika jijini Dodoma wakati Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikabidhi magari 17 kwa Idara ya Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu) na 13 kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).


“Kwa upande wa magari yaliyotumika muda mrefu ambayo yamekuwa mzigo kwa Serikali, maafisa masuhuli waangalie namna ya kuwakopesha au kuwauzia watumishi wanayoyahitaji kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo badala ya kuyaacha kwenye maegesho,” ameagiza Waziri Mkuu.


Pamoja na hilo, Mhe. Majaliwa amewaagiza maafisa usafiri wa Idara zote za Serikali wazingatie mpango maalum wa matengenezo ya magari kufanyika kwa wakati, kutumia vifaa vyenye ubora na kutunza taarifa za kila chombo. 


Naye, Mwakilishi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ameipongeza Serikali kwa kukabidhi magari hayo kwa taasisi hizo huku akitoa wito kwa wafanyakazi kuzingatia uadilifu katika utendaji kazi.








Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: