Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane 2023 Mkoani Shinyanga yamefanyika katika uwanja wa CCM Kambarage na kwamba  imefanyika michezo mbalimbali ya Baskeli kwa wanaume na wanawake.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Mkurugenzi wa CM Entertainment Bwana Clouds Malunde kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya SHY BEST ambapo washindi wa mbio za Baskeli wamepewa zawadi za fedha.

Kulwa Mahega ni mkazi wa kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga amekuwa msindi wa kwanza mbio za Baskeli kundi A ambapo amepewa zawadi ya Pikipiki mpya aina ya SANLG

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wamesema maadhimisho hayo ni chachu ya kuboresha shughuli za kilimo na uvuvi na kwamba wameomba yaendelea kuadhimishwa kila Mwaka.

Kauli mbiu ya maonyesho ya wakulima nane nane kwa Mwaka huu 2023 inasema vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula.

  

Maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane leo Agosti 8, 2023 yakiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na kwamba yameandaliwa na Mkurugenzi wa CM Entertainment Bwana Clouds Malunde.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: