Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule Ametoa Rai kwa wananchi jijini hapo kufuata taratibu za ujenzi kwani jiji hilo Limepangwa.

Senyamule ametoa Rai hiyo leo alipokua katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwaajili ya kuzindua Mkakati wa Mkoa wa kushughulikia migogoro ya Ardhi na kukiri kwamba wananchi wanajenga bila kufuata Masharti ya Ujenzi.

“Nitoe Wito kwa wananchi mtu anapotaka kujenga nyumba aende jiji kwani kuna suala la mabati kwamba eneo fulani kuwekwe bati za rangi fulani hivyo ni muhimu kwenda jiji ili kupewa taratibu hizo zilizopangwa kwa jiji let.”Ametoa Wito Senyamule

Senyamule Amesema wananchi wanapaswa kufuata taratibu za ardhi ikiwa ni kuacha kujenga nyumba zaidi ya moja katika kiwanja kimoja kwamba mwananchi kujenga nyumba ya kuishi na nyumba ya kupangisha   jambo ambalo haliruhusuwi na Mamlaka ya Ardhi.



Kadhalika Senyamule amesema yapo baadhi ya wananchi wanaojenga nyumba katika Mashable yaliyopangwa na jiji kutumika kama mashamba ambayo yanasaidia kupamba jiji na kuonesha muonekano wa jiji Pamoja na kuzalisha hewa.

“Jambo la kujenga kwenye maeneo ya mashamba haliruhusuwi na wala halifumbiwi macho kama mwananchi anataka kujenga awasiliane na jiji kupewa maelekezo na tukikuta mashamba hayo yamepandiwa mazao hilo sawa lakini siyo kujenga nyumba katika mashamba.” Amesisitiza Senyamule

Halmashauri ya Jiji la Dodoma kama ilivyo kwa halmashauri nyingine hapa nchini, kwa sasa ni moja ya halmashauri zinazokabiliwa na kero za migogoro mingi ya ardhi.

Kufuatia migogoro hiyo mingi Senyamule Amesema  kumekuwa na jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikichuliwa na halmashauri, ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa pamoja na  Wizara ya Ardhi na vyombo vingine vya utatuzi wa migogoro katika kuipatia ufumbuzi.


Kwa muda mrefu mamlaka mbalimbali za serikali zimekuwa zikijitahidi kutatua migogoro hiyo lakini imekuwa haiishi na wananchi kuendelea kulalamikia. 

Amesema kama Mkoa uchunguzi ulifanyika na kubaini malalamiko mengi ni ya fidia na watu walioahidiwa kupewa viwanja mbadala.  

“Kimsingi maelekezo mbalimbali yalikuwa yanatolewa ili kutafuta ufumbuzi wa suala hili lakini suluhu ilikuwa haipatikani kwa kuwa  Halmashauri ya Jiji ilikuwa haitoi kipaumbele katika kutenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia ikiwa ni pamoja na kupima viwanja kwa ajili ya kutoa kama mbadala wa kumaliza kero hizi.”Amesema Senyamule

Kwa Upande wake Mkuu wa  Wilaya ya  Dodoma Mh. Jabir Shekimweri Ametoa wito kwa Watumishi kutumika lugha nzuri kwa wateja wao ambao ni wananchi na kufanya kazi kwa hofu ya Mungu huku wakiheshimu watu .

Naye Mstahiki meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe Amesema mkakati huo utaleta mageuzi ndani ya Jiji na migogoro ya Ardhi kuisha Jijini Dodoma.


Ikumbukwe kuwa Tangu kutangazwa rasmi kwa Mpango wa Serikali wa kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma,Jiji limeendelea kukua  kwa kasi hivyo kwa mujibu wa makisio ya mwaka 2022 ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Jiji la Dodoma linakadiriwa kuwa na Wakazi takribani 765,179 ambao ni sawa na ongezeko la 16.2% la idadi ya wakazi wote waliokuwepo mwaka 2016. 

Ongezeko hilo limepelekea uwepo wa hitaji kubwa ardhi hususani la viwanja kwa ajili ya kukidhi matumizi ya shughuli za ofisi mbalimbali za umma na binafsi sambamba na biashara mpya zinazofunguliwa.




Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: