Kikao cha kujadili uanzishaji wa namba maalumu kwaajili ya utambuzi  ya utoaji huduma za serikali kimefanyika Jijini Arusha kikishirikisha Taasisi nyingine 
Kama  RITA, NIDA ,UHAMIAJI,ZCSRA -Zanzibar,UTUMISHI

Akizungumza  katika kikao hicho  Katibu Mkuu Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis alisema  siyo kwamba wanaanzisha namba nyingine bali wanafanya utaratibu wa  namba hiyo bali watakapomaliza majadiliano watakubaliana iwe inamtambulisha Mwananchi na mgeni yeyote atakayeingia nchini.

Aidha amesema kuwa Lengo kubwa la hizo Taasisi ni kupitia kwa pamoja kwani  wamenaanza safari ya uchumi wa kidigital kwa kuunganishwa kwenye mifumo mbalimbali kwa kujadili kwa  kiana ,kukubaliana na kupata wasilisho la kuwa na namba moja Jamii

"Tuna safari na niyakuipeleka tanzania kwenye uchumi wa kidigitali, na yapo mmbo mengi ya kufanya ili tuweze kufika kule, ili mwananchi aweze kufanya maendeleo lazima atambulike kwa Namba jamii'' Alisema

Aidha Katibu huyo alisema kuwa Namba Jamii hiyo siyo kitambulisho kipya  bali itamtambua mwananchi tangia anapozaliwa hadi anapoondoka duniani huku ikiwa imesheheni taarifa zake zote kikamilifu

Mkurugenzi wa TEHAMA Priscus P. Kiwango alisema kuwa Namba Jamii hiyo itasaidia kuwa na taarifa zote, kwa namba moja tofauti na ilivyo sasa na hiyo itaepusha usumbufu wa kuwa na mlundikano wa vitamulisho ambavyo ni vya mtu mmoja lakini vinamtambulisha tofauti.

Akijibu swali lililoulizwa na mwandishi Alan Isack  sliyetaka kujua Je mpango huu wa kuleta namba  hiyo haitaleta  mkwamo kutokana na Tanzania bara / Zanzibar kwani kila mmoja ana taratibu zake?: Ndiyo maana ya kunakaa kwa pamoja Taasisi ya Nida,Uhamiaji,Rita,Zcsra na Utumishi, tukubaliane kama serikali kwamba mmoja wao awe ndiye atatoa namba ili mwananchi  uweze kupata huduma.

"Kila mwanadamu ana mzunguko wa maisha na kwenye matukio hayo kuna taasisi inawajibika, mf. Hospitali, Rita kwenye vizazi na vifo, Uhamiaji kutambua uraia wa mtu lakini bado baadhi haziongei kwa pamoja ndiyo maana tuunajadili Juu ya Namba Jamii".alisema Katibu

Uzuri wa Taasisi ya Uhamiaji na NIDA ni Taasisi za Muungano, hivyo sisi tunataka mwananchi apate huduma akiwa kwenye ardhi ya Tanzania bara, au Visiwani,kuna baadhi ya huduma za serikali zinatumia namba ya NIDA na bila hiyo hupati huduma,hivyo wale ambao bado wajisajili au waanze mchakato mapema .

Swali jingine kutoka kwa Calvin Novat aliuliza Hili ni suala la kimfumo, je Tanzania imejipangaje kuingia katika mabadiliko haya ya kimfumo?:

Amesema kwenye masuala ya mifumo,Nchi ya Tanzania  imeanza kitambo, na baadhi ya mifumo wapo vizuri ila baadhi ya hiyo mifumo haiongei,wanachokitafuta wakienda kwenye mfumo A,B,na C iwe na utambuzi mmoja ambao majina hayatofautiani. 
Share To:

Post A Comment: