Na John Walter-Babati

Mbunge wa Babati Vijijni , Mwenyekiti wa Bunge na Mwenyekiti wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Daniel Sillo ameupiga Mwingi,  ndivyo unavyoweza kusema baada ya kutumia pesa zake za Mshahara kuboresha hali ya elimu, afya na miundombinu mingine katika wilaya ya Babati.

Kwa mwaka 2022-2023 pekee Mbunge huyo ametoa Mabati 150 kwa ajili ya Zahanati ya  Kijiji cha Tsamas, Mabati 117 Zahanati ya Luxmanda ambayo inaendelea kujengwa.

Aidha katika kipindi hicho hicho,  ametoa Mabati 110 shule ya Msingi Datar kata ya Ufana, Mabati 84 kata ya Boay kwa ajili ya Maabara,Mabati 29 kata ya Kisangaji ujenzi wa Maabara, Mabati 160 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Duru,Mabati 50 shule ya msingi Mandagew, Mabati 50 na viti sita vya walimu Shule ya Msingi Dohom, Mabati 50 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na kimbunga katika vijiji vya Bashnet na Nar.

Pia Sillo ameingia mfukoni kwake na kununua Mashine za kuchapisha ili zisaidie kutoa mitihani ya mara kwa mara na nyaraka zingine katika shule za Sekondari Gidas kata ya Gidas, Maganjwa kata ya Dabil, Galapo kata ya Galapo,Kisangaji, Gichameda kata ya Magugu, Burunge kata ya Nkaiti, Arrisaayo kata ya Arri,Masabeda kata ya Bashnet pamoja na Computer shule ya Sekondari Ufana na Kisangaji.

Ametoa Mifuko 30 ya Saruji ujenzi unaoendelea shule ya Sekondari Kiru six, Mifuko 10 ya Saruji shule ya Msingi Endasago, shilingi laki nne  ujenzi shule ya Msingi Ayamango.

Aidha katika kijiji cha Qameyu alichangia shilingi laki tatu kuwaunga mkono wananchi waliokuwa wakijitolea kutengeneza bara bara kwa mikono, shilingi laki mbili ujenzi wa josho kijiji cha Gabadaw  na Laki moja na sitini ujenzi wa shule ya msingi Ayatla.

Sillo amewaahidi Madiwani katika maeneo ambayo hajayagusa wawe na moyo wa subira kwani atawafikia wote.

Madiwani 25 wa Halmashauri ya wilaya ya Babati na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Anna Mbogo wamempongeza Mbunge huyo kwa kuwatumikia wananchi kwa moyo wa upendo.

Share To:

Post A Comment: