Na John Walter-Babati

Watumishi wa Serikali wilaya ya Babati mkoani Manyara  wameonywa tabia ya ulevi wakati wa saa za kazi pamoja na utoro bila sababu za msingi.

Onyo hilo limetolewa na Mkurugugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo  wakati akizungumza  katika baraza la madiwani leo Julai 27,2023.

Onyo hilo limekuja baada ya Diwani wa kata ya Kisangaji Adamu Ipingika kuliambia baraza hilo kuwa Afisa mtendaji wa kata hiyo anatumia muda mwingi kunywa pombe na kushindwa kufika kazini kuhudumia wananchi na kwamba ameshamuonya mara kadhaa bila mafanikio.

Mkurugenzi huyo amesema kuna baadhi ya watumishi wana tabia ya kunywa pombe na kulewa muda wa kazi na hivyo kushindwa kutoa huduma kwa wananchi kikamilifu.

Amesema ulevi kazini ni kosa na kuwataka wenye tabia hizo waache haraka kabla hawajachukuliwa hatua za stahiki.

Pia amesema hatotaka kuona watumishi watoro na wazembe kazini na kumpa muda afisa mtendaji kata ya Kisangaji kubadilika kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo amewataka Madiwani na watumishi wengine wa serikali  kuitendea haki nafasi waliyopewa ili wananchi wapate maendeleo.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya amemuhakikishia amesema madiwani katika kata zote 25 wanaendelea kutimiza majukumu yao ya kuwawakilisha wananchi waliowachagua.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya akizungumza katika baraza la Madiwani lililoketi leo.

Share To:

Post A Comment: