Jumuiya ya wanafunzi Taasisi ya elimu ya juu Tanzania, vyuo vya kati
na vyuo vikuu Mkoa wa Tabora wameiomba serikali kuendelea kutoa fursa za ajira,
kutambua na kukuza vipaji vya watoto wenye ulemavu Nchini.
Kauli hiyo imetolewa na makamu wa Rais
mstaafu wa serikali ya wanachuo katika chuo kikuu kishiriki cha Askofu mkuu Mihayo
Tabora, Jojina Nyamboko baada ya
kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wanaolelewa katika
kituo cha Buhangija jumuishi katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa jumuiya
ya wanafunzi Taasisi ya elimu ya juu Bi. Maria Thomas, Jojina Nyamboko ambaye
pia ni kamishna wa watu wenye mahitaji maalum TAHLISO ameiomba serikali
kuwatambua watu wenye ulemavu kwa nafasi, vipaji na uwezo wao hasa wale wanaohitimu katika
vyuo mbalimbali Nchini.
“Ombi langu kwa serikali tujaribu kuwatambua watu
wenye mahitaji maalum kwa nafasi zao na uwezo wao wapo watu wanamaliza vyuo
wanauwezo kwahiyo namuomba mama yetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akumbuke
kwamba hawa watu wenye mahitaji maalum kwa vile wanavipaji tofauti tofauti hata
anavyokuwa anatoa teuzi akumbuke pia kuwaweka watu wenye mahitaji maalum wakiwa
pale ni mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wataendelea kuhamasisha watu
wenye mahitaji maalum wengine kujitokeza na kuendelea kusoma ili wapate taaluma
mbalimbali na kuendelea kuisaidia jamii”.Amesema Jojina
Ametaja malengo mbalimbali yaliyosababisha
wanavyuo hao kufika na kutoa msaada katika kituo hicho kwamba ni pamoja na
kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kusoma na kujifunza ili waweze kufikia malengo
yao, kuwaonyesha upendo watoto hao, kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia
katika kujenga jamii jumuishi.
Aidha kamishna wa watu wenye mahitaji
maalum TAHLISO Georgina Nyamboko ametumia nafasi hiyo kuipongeza serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kuboresha miundominu ya elimu kwenye vituo vya wanafunzi wenye mahitaji maalum
Nchini.
Wakizungumza na wanafunzi hao baadhi ya
viongozi wa vyuo wametumia nafasi hiyo kuwasisitiza kuongeza juhudi katika
masomo ili waweze kukabiliana na mazingira ya sasa yanayohitaji wasomi na wataakam
waliobobea.
Katika ziara hiyo wameongozana na wanachuo
wenye mahitaji maalum kutoka Mkoa wa Tabora ambapo pia pamoja na mambo mengine
wametoa elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa maadili ili
kuepuka vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti.
“Tumeona
pia tutoe elimu namna ya kukabiliana na changamoto ya kuporomoka kwa maadili
hasa ya vijana, tumeona sahzi maporomoko ya maadili yamekuwa mengi hasa
ubakaji, uvutaji wa madawa ya kulevya pamoja ya ushoga wao kama watu wenye changamoto
unakuta mwengine haoni je anawezaje kuishi kwenye jamii hii ambayo imeporomoka
kwenye maadili”.amesema Jojina
Akizungumza kwa niamba ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Shinyanga , Afisa elimu Halmashauri hiyo Mwalimu Wingwila Kitila
ameshukuru na kuwapongeza wanachuo hao kwa kuguswa na changamoto zilizopo
kwenye kituo cha Buhangija jumuishi.
Jumuiya ya wanafunzi Taasisi ya elimu ya juu Tanzania, vyuo vya kati na vyuo vikuu Mkoa wa Tabora wamefanya ziara ya kuwatembelea wa shule ya msingi Buhangija ambapo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Sabuni, Dawa za mswaki, Madafutari, Taulo za kike, Viatu, Juice pamoja na kupanda miti 50 katika eneo la shule hiyo.
Hafla ya kukabidhi msaada kwa watoto wenye
mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga ikiendelea.
Hafla ya kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga ikiendelea.
Hafla ya kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga ikiendelea.
Zoezi la kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji
shule ya Buhangija Mjini Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga likiendelea.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada
kwa watoto wenye mahitaji shule ya Buhangija Mjini Shinyanga.

Post A Comment: