Na Gift Mongi ; DODOMA


Huenda wakulima wa zao la kahawa Kwa sasa wakawa na matumaini katika zao hilo kutoka a na jitihada za wazi zilizoainishwa na serikali katika 

Hivi sasa SERIKALI kupitia wizara ya Kilimo imeahidi kuendelea kuzalisha miche bora ya zao la kahawa yenye ukinzani dhidi ya magonjwa sugu ya kahawa.

Kauli hiyo inetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi alilohoji je Serikali ina mpango gani wa kuendelea kusambaza miche bora ya kahawa yenye sifa ya ukinzani wa magonjwa sugu ya kahawa katika jimbo la Moshi vijijini.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mavunde alisema kuwa, kwa sababu mibuni iliyopo asilimia kubwa imeshakaa zaidi ya miaka 25 na hivyo kupunguza uzalishaji hivi sasa Serikali kupitia Tacri na Bodi ya Kahawa watahakikisha wanazalisha miche ya kutosha .

Alisema kuwa, kwa sasa wanatumia Teknolojia ya chupa ili wakulima wengi zaidi wapate miche na iwafikie kwa urahisi na waweze kuongeza uzalishaji ikiwemo wakulima wa Jimbo la Moshi vijijini.

Hatua hiyo ni neema kubwa kwa wakulima wa zao la kahawa nchi ambalo limekuwa likichangia kuongeza pato la Taifa na kuingizia fedha za kigeni.


Share To:

Post A Comment: