Na Gift Mongi : Moshi

Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa na mazingira rafiki yakujisomea serikali imefadhili ujenzi wa madarasa manne na bweni moja   la  kulala katika shule ya sekondari ya wasichana  Weruweru iliyjopo Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mbunge wa jimbo hilo Prof Patrick Ndakidemi kwa kupitia taarifa yake kwenda kwenye vyombo vya habari inaeleza kuwa  ujenzi huu uko katika hatua za mwisho kamilika (98%). 

'Katika mradi huu mabweni yatawekwa vitanda na madarasa yatapata madawati ujenzi huo umegharimu Shilingi milioni 280.'anaeleza na kuongeza

'Tunamshukuru sana Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha  kuboresha shule hii kongwe hapa nchini. '

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa jimbo la Moshi Vijijini waliopo karibu na shule hiyo Andrew Mushi amesema serikali kwa sasa imekuwa ikapanua wigo kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi kusoma na kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali.

'Kipekee tumshukuru rais Dkt Samia kwa maoni yake katika kuboresha shule hii kongwe ambayo Ina historia ya kipekee katika kuzalisha viongozi'anasema

Ameongeza pia hata kuwezeshwa kujengwa kwa madarasa hayo na bweni ni matokeo ya mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ambapo kwa mara kadhaa amekuwa akitetea maslahi ya wakazi wa jimbo lake.

Ruth Mallya anasema kuwa shule hiyo na kama zilivyo shule nyingine zipo katika historia ya kipekee katika kuzalisha viongozi mbali mbali hapa nchini hivyo kukumbuka ni sehemu ya kuitukunuku.

'Hii shule ni kama tanuru la kutoka viongozi hivyo kama isingekarabatiwa ni sawa na kama ingekuwa imetelekezwa ila kipekee tuishukuru serikali kwa haya yaliyofanyika ni jambo jema' anasema

Share To:

Post A Comment: