Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Njombe imelaani na kukemea vikali kauli ya ubaguzi inayofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani na wafuasi wao.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Njombe Samwel Mgaya,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,alisema jambo hilo linavuruga na kutia hofu kama taifa,kwa kutoa lugha hatarishi zinazolenga kuharisha umoja wa kitaifa na kuchochea ubaguzi katika jamii.

"Sisi vijana tumechukulia kauli hizo za ubaguzi kwa taadhari kubwa sana"alisema Mgaya.

Mgaya alisema mjadala uliokuwa unaendelea kuhusu kuwa na makubaliano ya serikali na serikali ya Dubai kabla ya kujadiliwa ubungeni kwa ajili ya kupitisha azimio ili kuweka misingi kuwepo kwa mikataba ya uendelezaji na uboreshaji wa uendashaji wa bandari nchini,kuna wanasiasa wametumia mwanya huo kutoa Lugha na maneno ya ubaguzi wa wazi kabisa.

"Kupitia kile alichokiita ni mkutano na waandishi wa habari(usiku wa manane?),katika video fupi(clip)ambayo imesambaa mtandaoni,kiongozi mmoja mkubwa tu wa chama cha siasa amesikika waziwazi akitoa kauli za ubaguzi dhidi ya watanzania wanaotokea Zanzibar,tena akiwalenga watu kwa majina na nafasi zao wanazotumikia katika uongozi"alisema Mgaya.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan yupo kazini katika kuhakikisha kwamba nchi inabadilika kuendana na kasi ya teknolojia.

"Suala la bandari,bandari yetu inategemewa na nchi nyingi kwa hiyo uhitaji wa mizigo kitoka nchi za jirani ni mkubwa kuliko huduma zinazopatikana bandarini"alisema Mgaya.

Share To:

Post A Comment: