Na Mwandishi wetu - Kagera

Wataalam kutoka Wizara za kisekta chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza uchunguzi wa Kiikolojia kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Marburg baada ya ugonjwa huo kutokomezwa Nchini.

 Wataalamu wanaounda timu wanatoka ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ofisi ya Waziri Mkuu ( Menejimenti ya Maafa), Wizara ya 
 Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (TAWIRI), na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI)

Watalam hao ambao wamekutana Mkoani Kagera wanalenga mufanya uchunguzi wa kiikolojia ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kimataifa ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za ufuatiliaji baada ya ugonjwa huo kutoweka.

Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Prudence Constantine amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imeratibu sekta na Taasisi mbalimbali kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg na mwingiliano wao na wanadamu ambapo Uchunguzi huu ni moja kati ya juhudi za pamoja za kuendelea kujua chanzo cha tatizo, kujiandaa, kukabiliana na dharura za kiafya ikiwemo endapo zitajitokeza.


"Wizara ya Afya imeainisha uchunguzi huu kati ya kazi muhimu zinazotakiwa kufanyika ndani ya mpango wa siku 90 wa kurejesha hali Mara baada ya mlipuko wa Marburg ulipotangazwa kuisha".ameeleza Mkurugenzi Prudence 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera ,Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Issessanda Kaniki amesema baada ufuatiliaji wa mbinu za utafiti na vipimo ndani ya siku 42 tumeweza kuudhibiti ugonjwa huo hivyo hadi sasa hakuna Mgonjwa hata mmoja.


"Baada ya Ufuatiliaji lakini pia na mbinu mbalimbali za Utafiti Mkoa wa Kagera pamoja na Nchi tunazopakana nazo kwa sasa mlipuko wa Ugonjwa wa Marburg haupo tena".Amesema Dkt. Kaniki.

Uchunguzi huu wa Kiikolojia utakaofanyika kati ya tarehe 12 na 24 Juni, 2023 utahusisha uchukuaji wa sampuli za Wanyamapori, wanyama wa kufugwa pamoja na kufanya utafiti shirikishi jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Muleba na Kyerwa.

                Mkurugenzi Msaidizi Tiba na Mratibu Tafiti Wizara ya Afya Dkt. Pius Horumpende akitoa muongozo kuhusu Ziara hiyo.



        
           Baadhi ya Wataalamu waliopo kwenye ziara hiyo.



(PICHA ZOTE OFISI YA WAZIRI MKUU)
Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: