Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na maafisa ustawi wa jamii wametoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga ambao wapo kwenye kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM.

SMAUJATA ni kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia  Nchini Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2022 chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu ambayo inayosimamiwa na Waziri Dkt. Dorothy Gwajima.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi emetoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi hao huku akiwasisitiza kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa za ukatili unaoendelea kufanyika katika jamii hasa wawapo shuleni ili kutokomeza vitendo hivyo.

Madam Kisendi ametaja aina mbalimbali za ukatili ikiwemo ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa kingono ambapo amewasihi wanafunzi hao kuepuka ukatili na kwamba amewasisitiza kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao.

“Kuna ukatili wa kimwili unafanyika huko shuleni ninyi msikubali kufanyiwa lakini pia ukatili wa kijinsia msikubali haya yafanyike mkiona mtoto anafanyiwa vitendo vya ukatili toa taarifa au piga simu namba ya bure kabisa ya serikali ambayo ni 116 lakini kuna viongozi wa vijiji, mitaa watendaji na maafisa ustawi wa jamii mtoe huko taarifa”.

“Kwa umri wetu huu mnatakiwi kusoma kwa bidii ili mtimize ndoto zenu achana na huu ukatili wa kingono utapata ujauzito na hizi ni mimba za utotoni ambazo zinakatisha malengo ya watu wengi kwahiyo msifanye mapenzi mkiwa na umri mdogo someni kwanza hayo mambo kuna wakati wake”.amesema Mwenyekiti Madam Kisendi

Katika hatua nyingine afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo ubakaji na  ulawiti ambapo amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuzingatia taratibu na miongozi zilizopo shuleni ili waweze kumaliza masomo yao salama.

Aidha baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga akiwemo makamu mwenyekiti wa kampeni hiyo Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Vicent  Kanyogota nao wametoa elimu juu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanya.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga wameshukuru na kuwapongeza viongozi wa kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu hiyo ambapo wameahidi kuwa mabalozi wazuri wa kupinga ukatili hasa wawapo shuleni.

Nao baadhi ya walimu na walezi wa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga wamepongeza kwa elimu hiyo huku wakiwaomba viongozi wa kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na maafisa ustawi wa jamii kuendelea kutoa elimu hiyo ya ukatili kwenye shule mbalimbali ili kudhibiti ukatili wanaofanyiwa wanafunzi aidha bila wao kujua.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Mwenyekiti idara ya wanawake SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga  Bi. Esther Emmanuel akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: