Na Mapuli Misalaba

Waziri wa  maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wazazi, walezi na jamii kuwajibika kwenye suala la malezi ikiwa ni pamoja na matunzo na ulinzi wa mtoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.

Akifungua maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma ambayo yamekwenda sanjari na sherehe za kampeni ya kupinga ukatili SMAUJATA kutimiza Mwaka mmoja tangu kuanzishwa Mwaka jana Juni 16.

 Pamoja na mambo mengine Dkt. Gwajima ametumia nafasi hiyo kuipongeza kampeni ya SMAUJATA kwa kuendelea kuisaidia serikali kupinga ukatili huku akiwasisitiza wazazi na walezi kuimarisha ulinzi wa watoto ili kuwaepusha na wimbi la watoto wa mitaani.

Amesema serikali itaendelea kusimamia sheria za mtoto ambapo amewaasa wazazi na walezi kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi baada ya watoto kupotea ili kuepuka changamoto.

“Ipo haja ya kufahamu kwa kija iwapo miongozo na mifumo ya kuwatambua watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ipo na je ipo imara au inaulegevu sehemu gani kwa sababu tunaendelea kuwaona watoto mitaani tutafanya zoezi kubwa la kubaini wapi mifumo hii inalegea tuchukue hatu”.

“Wazazi, walezi na jamii muwajibike kwenye malezi na matunzo ya watoto ili familia zao ziweze kuishi vizuri na watoto wafurahie maisha yao”.

“Sisi tukimpata mtoto yupo mtaani tunanchukua tunampa Juice atusimulie alifikaje hapo lakini tukirudi kwa wewe mzazi ambaye unatuambia mtoto wako haonekani miezi mitatu utuonyeshe RB ya Polisi, mzazi mmoja akipoteza Ng’ombe na kuku atawasumbua mno polisi halafu mzazi mmoja hamuoni mtoto wake wiki au mwezi analala tu usingizi hii maana yake nini anaenda kumtumikisha yule mtoto apate faida kama kweli anauchungu aende polisi akachukue RB tujue mtoto wake amepotea sisi tukimkamata mtoto mtaani tukaja kwako hauna RB tunakusomea sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 imefanyiwa marekebisho mwaka 2011 ukapambane na vifungu halali vya sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.amesema Dkt. Gwajima

Waziri Dkt. Dorothy Gwajima amewasisitiza watoto kuzisimamia haki zao kwa kufuata taratibu na sheria za Nchi ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu wazazi ambapo pia amewataka kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vya ukatili.

Mwenyekiti wa kampeni ya Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Bwana Sospeter Mosewe Bulugu amesema kampeni hiyo pia imejipanga kuhamasisha makazi bora ya wananchi, huduma bora kwa wazee, malezi pamoja na makuzi kwa watoto, misingi ya haki na usawa wa kijinsia sambamba na kuamsha ari ya wananchi katika uwekezaji, biashara na kilimo.

Mwenyekiti huyo amesema shughuli za kampeni ya SMAUJATA ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano ya ukatili Nchini kupitia sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuendana na kasi ya mabadiliko katika jamii na nyanja zingine mbalimbali.

Bwana Buluhu amesema mpaka sasa zaidi ya watanzania elfu kumi (10,098) wamejiunga na kampeni hiyo ya SMAUJATA ambapo pia amesema kwa muda wa Mwaka mmoja yapo mafanikio mbalimbali ikiwemo kusajiri shirika la Responsible Society Organization (RSO) na kwamba shirika hilo litashirikiana na wadau wengine katika shughuli za kupinga ukatili kwa mujibu wa sheria na taratibu za Nchi.

Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi OR – TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje amesema serikali itaendeleza mifumo ya ulinzi na usalama wa mtoto pamoja na kutoa elimu ili kuimarisha usalama.

“Moja ya mambo tunayoenda kuyafanyia kazi ni kuendeleza mifumo ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa kutumia kamati zile za ulinzi na usalama ngazi ya vijiji na mitaa lakini pia tutaendelea kuwatumia SMAUJATA ambao wapo kwenye ngazi ya vijiji ili kuhakikisha kwamba ulinzi wa watoto unaendelea kuimarika”.amesema Bi. Kabuje

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani inasema “Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidijitali”.

Waziri wa  maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo Ijumaa Juni 16,2023.


Mkurugenzi msaidizi OR – TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo Ijumaa Juni 16,2023.

Mwenyekiti wa kampeni ya Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Bwana Sospeter Mosewe Bulugu akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo Ijumaa Juni 16,2023.

 

Awali maadamano ya siku ya mtoto wa afrika kitaifa yakifanyika jiji Dodoma leo Ijumaa Juni 16,2023 kauli mbiu “Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidijitali”.



Share To:

Misalaba

Post A Comment: