Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP Umeandaa Mafunzo ya kuwajengea uewezo wanahabari wa vyombo vya Habari vya kijamii kuhusu wa namna bora ya  kuripoti Habari zinazohusu wanawake katika masuala ya  uongozi.


Mafunzo hayo yananyikia kwa siku mbili Jijini Dodoma kuanzia leo Juni 16 - 17, 2023 kuwapa uelewa wa namna gani Mwandishi wa Habari anamchango wa kushiriki na kuchangia katika masuala ya uongozi bora.

Akizingumza na waandishi  waliohudhuria Mafunzo hayo muwezeshaji Ananilea Nkya  Amesema Mwanahabari anaweza kumsaidia kiongozi kwa kufanya tafiti kwani kiongozi husika anapoona hizo taarifa  katika chombo Cha Habari husika anaweza akafanya jitihada ya kulitatua changamoto kwa kupitia tafiti hizo. 


"Sisi wanahabari tuna fursa ya kupita Vijiini kuona mambo ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwa ubora na ukamfanyia mahojiano huyo kiongozi alajua namna ya kulitatua hilo changamoto kupitia kwa Mwandishi kwahiyo  kupitia kazi yetu pia inaweza kusaidia viongozi wakawa na mbinu kutokana na sisi wenyewe tukiandika Habari za kuwasaidia kuwa na mbinu".

Ametoa rai kwa waandishi wa Habari kutumia lugha fasaha katika uandishi wao pamoja na kuangalia usawa  ili Habari zao ziweze kuleta maana katika jamii.

NKYA,  amesema,Waandishi wa Habari wananafasi kubwa katika jamii Kuondoa mitazamo hasi iliyopo kwenye jamii juu ya mwanamke ambayo inamkandamiza mwanamke katika kugombea nafasi mbalimbali katika jamii


"Kama tutaweza kuandika habari za kuwainua wanawake katika masuala ya uongozi tutaweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii inayowazunguka kwakuwa mwanamke anasifa kuu ya uongozi ambayo ni uoga hivyo hataweza kutumia vibaya uongozi wake".

Kwa upande wake Catherine Mzurikwao kutoka TGNP amesema waandishi wa Habari lazima wabadili misemo hasi iliyopo katika jamii kuhusiana na Suala Zima la mwanamke kuwa kiongozi.


"Kuna misemo hasi inayohusu wanawake na uongozi kwamba wanawake hawapendani  sasa waandishi wa Habari mnaongeleaje misemo ambayo inamuweka chini mwanamke na kufanya iwe chanya?".


SAIDA ISSA , Mwanahabari wa gazeti la Zanziba Leo , anasema Mitazamo hasi katika jamii imekuwa kikwazo kikubwa Kwa wanawake wengi kuchangamkia fursa mbalimbali za uongozi Kwa kuwa ni nikandamizi kwake hivyo akiwa mwandishi wahabari anajukimu kubwa na kuhakikisha jamii inaondoa mitazamo hasi na kumuona mwanamke.








Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: