DENIS CHAMBI, TANGA.

Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya jiji la Tanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwenye vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo katika kituo cha Nyumba ya furaha imetoa kilo 20 za mchele, kilo 40 za Maharage na vyandarua 10  wakivipatia vituo 6 vilivyopo hii ikiwa ni njia ya kuonyesha kuwajali na kuwathamini watoto hao.


Akizungumza katika kituo hicho katibu tawala wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya amewataka wazazi , walezi na jamii kwa ujumla kusimamia majukumu yao ipasavyo kwa watoto wakiwalinda na athari mbalimbali ikiwemo ukatili pamoja na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Alisema kutokana na mabadiliko ya kidigital Dunia imebadilika  sambamba na matukio mengi ya kiukatili dhidi ya watoto yakishamiri hivyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanakiandaa kizazi ambacho kitakuwa ni tegemeo la kesho. 

"Wazazi walezi tunapaswa kujua kwamba mtoto naye ana haki yake, ikiwemo kusikilizwa, kulindwa na kuangaliwa kwa umakini niwaombe sana wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia usalama wa  mtoto hakikisheni mnasimamia maadili ya mtoto kuanzia nyumbani, na sisi tunatamani tuwe na Taifa lenye vijana waadilifu baadaye  ambao watalisongeza taifa letu mbele linaendelea ya kiuchumi"

"Kuna mambo sasa hivi yanayoendelea katika jamii ni mengi dunia imeahabadilika tupo kwenye mfumo wa kidigital kuna mambo mengi yanafanyika wakati huu ikiwemo ukatili kwa watoto ,unyanyasaji , ubakaji, matumizi mabaya ya mitandao kuna Uhuru mkubwa sana upo kwa watoto, alisema Mikaya.

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa jiji la Tanga Simon Mdende alisema bado hali ya unyanyasaji kwa watoto katika jamii sii shwari licha ya elimu wanayoendelea kutoa  katika jamii kwa mslahi ya mtoto huku akiwataka wahisani mbalimbali kujitokeza kuvisaidia vituo vinavyolea watoto ili waweze kupata malezi na huduma bora wanazostahili.

"Katika halmashauri ya jiji la Tanga kwa watoto wanaoishi kwenye halmashauri ya jiji la Tanga hali sii nzuri sana kwasababu watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wamechukuliwa kutoka sehemu tofauti tofauti  wengi tunapowatoa kwenye mazingira waliyozoea wanaathirika kisaikolojia, katika hivi vituo wanapoishi Hawa watoto bado uchumi sio mzuri sana kwahiyo jamii inahitajika sana kujitoa na kusaidia hawa watoto ili kupata huduma mbalimbali" alisema Mdende.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jiji la Tanga Deogratias Casmiri amewataka wazazi na walezi pamoja na majukumu mengine kukaa karibu na watoto kubaini changamoto zinazowakabili katika mazingira ya nyumbani na mashuleni na hatimaye kuzitatua mapema kabla hawajaathirika kwa namna yeyote ile ili kuwa na kizazi bora Cha baadaye.

"Tusipoweka nguvu ya kutosha katika malezi ya watoto tutakuwa huo ustawi wa watoto hatuupati, ustawi wa mtoto maana take apate huduma zote za msingi ikiwemo chakula, malazi, elimu muda wa kukaa karibu na wazazi, walezi wake , Usimamizi wa haki za mtoto unaanzia kwa mazazi mlezi na jamii yote kwa ujumla  kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu jukumu la kuwaangalia watoto ni la kila raia" alisema Casmiri.

Wakizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo mkurugenzi wa kituo cha  Goodwill and foundation  Sayid  Muhzari Aidarus na mlezi wa kituo cha Nyumba ya Furaha Sister  Sarah Francis  wameeleza hisia zao  juu ya msaada hi uliotolewa na halmashauri wakiwataka wadau na wahisani mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia watoto waliopo katika vituo hivyo hii Ni kutokana na mahitaji yao huku vituo vikielemewa kutokana na uchumi mdogo.

"Kwa niaba ya taasisi niwapongeze na niwashukuru sana kwaajili ya tukio hili adhimu na lenye thamani juu ya mtoto, watoto Hawa Wana ufahamu na pale wanapoona jamii haiitikii kuja kwao wanahisi kwamba wametengwa  kwahiyo tusipokuja Kama hivi Tutajenga Taifa la watu wenye roho mbaya na roho ngumu kwa sababu wataona hawapotezi chochote kwahiyo kuja kqenu mmewakilisha mamilioni ya watanzania" alisema Aidarus.

"Kwa niaba ya masister na watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha tunashukuru sana kwa  yale yote ambayo mmetutendea Kama serikali katika kituo chetu na vituo vyote ambavyo mnatoa misaada hii Hawa watoto tuliokuwepo nao Wana mahitaji ya vitu vingi na hqki zao za msingi zinatakiwa zitolewe Kama watoto wengine  waliolelewa na wazazi wawili" alisema Sister Sarah.

Siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo June 16 na mwaka huu umebebwa na kauli mbiu ya "Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidigital".
 
Katibu tawala wilaya ya Tanga Mikaya Dalmia kimkabidhi mmoja wa watoto wanaolele katika kituo cha malezi cha Nyumba ya Furaha Net kilichopo jijini Tanga za Mbu zilizotolewa na halmashauri ya jiji la Tanga kwenye madhimisho ya siku ya mtoto wa wa Afrika.


Mlezi wa kituo cha masista cha Nyumba ta Furaha akzungumza mara baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula vilivyotolewa na halmashauri ya jiji la Tanga kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa kila mwaka june 16.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Simon Mdende halmashauri ya jiji la Tanga akizungumza  mara baada ya kukabidhi vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa vituo sita vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Goodwill anfa Foundation Sayid  Muhzari Aidarus akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula vilivyotolewa na halmashauri ya jiji la Tanga kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa kila mwaka june 16.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha malezi cha chumba ya Furaha iliyopo jijini Tanga akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula vilivyotolewa na halmashauri ya jiji la Tanga kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa kila mwaka june 16.
 

 

Share To:

Post A Comment: