NA DENIS CHAMBI, TANGA.

 MFANYABIASHARA maarufu jijini Tanga aliyefahamika kwa jina Hamis Rashid (53) mapema leo june 27,2023 amekutwa amefariki katika chumba chake cha kuhifadhiwa vitu  ' Stoo' baada ya kujinyonga kwa kutumia waya wa umeme  huku chanzo cha kuchukuwa uamuzi huo kikiwa  bado hakijulikani.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari  kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga  Henry Mwaibambe alisema walipata taarifa   kutoka kwa mke wa marehem aliyefahamika kwa jina la  Mwanaidi Issa  na kusema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo hicho.

"Mtu mmoja mfanyabiashara maarufu aliyefahamika kwa jina la Hamis Rashid amekutwa amejinyonga katika chumba chake cha stoo mpaka sasa hatujajua sababu gani iliyosababisha achukue uamuzi huo, kwenye chumba chake tumekuta kwamba alijaribu kujinyonga mara tatu kachukua kamba ya kwanza imekatika , ya pili ikawa imekatika  akakata waya wa umeme ndio amajinyonya nao"

 "Tarifa hizi tumezipata kutoka  kwa mke wake  anaitwa Mwanaidi Issa hatujajua chanzo cha kujichukulia uamuzi huo ni nini, lakini uchunguzi unaendelea tutajua mwisho nini kilisababisha achukue uamuzi huo" alisema Kamanda Mwaibambe.

Katika tukio lingine Kamanda  alisema kuwa mapema leo june 27, 2023  mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Damian Pius  mkazi wa Amboni mwenye umri wa miaka 24 dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda amekutwa ameuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali  na watu wasiojulikana taarifa za mashuhuda zikieleza kuwa alikuwa amebeba  gunia la mkaa ambalo  chini yake kulikuwa na Mirungi.

"Vile vile mapema leo tuna tukio la mauaji  eneo la barabara ya Utofu Chumbageni mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la  Damian Pius (24)  huyu Ni boda boda amekutwa ameuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani  lakini eneo la tukio tuliona Kama kulikuwa na vurugu, taarifa za mashuhuda Ni kwamba  huyu mtu alikuwa na gunia la mkaa na chini yake  kukawa na mirungi  waliokuwa wanagombania hiyo mirungi na mwenzake mmoja akampiga na hiyo nondo"

"Kwahiyo tumemkamata  mtu mmoja anaitwa Oscar Steven Haule (26)  ambaye naye Ni bodaboda mwenzake  upelelezi zaidi wa tukio hilo unaendelea" aliongeza Kamanda Mwaibambe.

Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi badala take kuwafikisha wahalifu kwenye vyombo vya dola pale wanapoona matukio karibu na makazi yao.



Share To:

Post A Comment: