NA DENIS CHAMBI, TANGA.

Taasisi ya mfuko Self Microfinance inayojihusisha na ukopeshaji wa fedha imefanikiwa kuyagusa makundi mbalimbali na shughuli wanazozifanya wananchi hii ikiwa na lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi pale ambapo taasisi na mtu binafsi atahitaji kujiendeleza ili kupata faida  zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga afisa mfawidhi wa  mfuko wa Self Microfinance Julius Mungengele alisema ni lengo la taasisi hiyo kumfikia kila mteja kulingana na shughuli anayoifanya, taasisi  na watu binafsi wenye vigezo ya kuweza kupata mikopo hiyo yenye riba nafuu pale ambapo watajiridhisha mteja wao anakidhi kupata mikopo wanayotoa.

" Lengo kuu la kutoa mkopo kwa mtu hasa ni  kumsaidia na sisi tunataka aonyeshe nia kweli ya kutaka kubadilika na sisi riba yetu ni nafuu na rafiki kwa  kila  mteja cha kusistiza tu ni kwamba lazima mteja azingatie  vigezo na masharti ikiwemo   muda  wa mkopo wake"

Mungengele   alizitaja huduma ambazo wanatoa kwa wateja wao ambazo ni pamoja na mikopo ya kilimo , mkopo wa mkulima, biashara , Imarika, amtaji, mkopo wa mshahara ambazo wanazitoa  kwa riba nafuu kwa wanufaika wao.

"Miongoni mwa huduma ambazo Self Microfinance finance tunazitoa na zimewanufaisha wateja wetu na zimegusa zaidi jamii ya watu wa hali ya chini ni mkopo wa mkulima, mkopo wa kilimo na mtaji lakini pia tunatoa mikopo hii kwa riba nafuu hasa ya mshabara, biashara na mkopo wa Imarika" alisema Mungengele.

Aidha aliwataka wananchi hususani  wenye sifa za mikopo zikiwemo wadhamini, mali inayodhaminika ,leseni za biashara na vitambulisho vinavyomtambulisha  mnufaika kufika katika mabanda  hasa kipindi hiki cha maonyesho ya baishara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako ili kupata elimu zaidi.

Pamoja na hayo alisema  mfuko Self  Microfinance unaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika kujiendeleza kiuchumi kupitia sekta ya kilimo biashara huku   akiwataka kuchangamkia fursa zinazopatikana ili kuweza kujiletea maendeleo.

Maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika mkoani Tanga ambayo ni ya 10  mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo ‘Kilimo , viwanda utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’
Afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance mkoa wa Tanga  Julius Mungengele akitoa elimu kwa Abdul Faraji ambaye ni mmoja wa wateja waliofika katika banda lao kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja v ya Mwahako.
 
Afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance mkoa wa Tanga  Julius Mungengele akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya baiashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya mwahako.

Afisa mfawidhi wa mfuko wa Self Microfinance mkoa wa Tanga  Julius Mungengele akitoa elimu kwa wanafunzi wa shulke za msingi waliotembelea banda hilo  kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako.


Share To:

Post A Comment: