NA DENIS CHAMBI, TANGA.

ZAIDI ya watalii Million 1.2 kutoka mataifa mbalimbali wametembelea vivutio mbalimbali vilivyopo haa nchini kwa kipindi cha mwaka 2022 hii ikiwa ni idadi kubwa kuywahi kutokea janga la ugojwa wa COVID – 19 ambapo sekta ya utalii kwa asilimia kubwa .

Hayo yamebai nishwa na afisa utalii kutoka bodi ya utalii Tanzania William Halule wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kufanyika  mkoani Tanga ambayo hujumuisha makampuni taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali  kwa lengo la kutangaza biashara na huduma wanazozitoa kwa jamii.

Alisema kuwa licha ya mlipuko wa janga la COVID -19 na hata baada ya  ugonjwa huo bado watalii walimiminika kutoka mataifa mbalimbali kuja kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi mbalimbali hapa nchini ambapo pia ilichagizwa na uzinduzi wa filamu ya Royal tour iliyozinduliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan alipokuwa nchini Marekani.

“Muitikio ni mkubwa sana baada ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan kufanya Royal tour  kweli wazungu wameongezeka sana kama mwaka jana  tumepata watalii Million  1.2 tulitoka kwenye ugonjwa wa COVID -19 lakini bado tukapata watalii wengi  hii ilitokana na ziara ile ya Rais kutangaza Roayal  tour “alisema

 Kwa upande wake afisa utalii kutoka hifadhi za Taifa Tanzania   'TANAPA' Athumani Mbaye lisema hifadhi zote zinazosimamiwa na TANAPA zimekuwa zikipata watalii wengi wa ndani na nje hii ikisadifu matokeo na hamasa kubwa iliyopayikana kupitia filamu ya Royal tour iliuofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni jitihada za serikali ya awamu  ya 6 kuzitangaza Tanzania kimataifa kupitia sekta ya utalii.

 "Kwa kweli utalii unakuwa siku hadi siku na hii inayokana na juhudi kubwa ambazo zinafanywa na shirika la hifadhi za Tanzania  "TANAPA" lakini pia kupitia Royal tour ambayo aliizindua Rais Samia Suluhu Hassan  amefanya juhudi kubwa kuzitangaza hizi hifadhi tangu ametoa hiyo filamu utalii umekuwa na tumejulikana sana  kimataifa tunapata wageni wengi kutoka nje  lakini pia na watalii wa ndani watanzania wenyewe  wamekuwa na muamko  kwa kuona kwamba Rais wetu anaweka juhudi kubwa katika sekta ya utalii" alisema Mbae.

 Alisema licha ya ongezeko watalii wa ndani na nje kuongezeka kumekuwa na changamoto ya miundombinu mibovu hasa kipindi cha mvua barabara zimekuwa hazipitiki kiurahisi  hata hivyo serikali iliona hilo hivyo  ambqpo iliyoa fedha kwaajili ya ukarabatI wa barabara zote ili kuhakikisha zinapitika kiurahisi.

 " Changamoto kama miundombinu wakati wa masika linakuwa na shida kwamba ufikikaji wa maeneo ya hifadhi kidogo  barabara  zinaleta shida lakini serikali inaleta fedha nyingi za kurekebisha hizo barabara  kwa sasa hivi barabara  zote zinapitika kwa muda wote" akiongeza

 Alisema kupitia maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga  yamekuwa na tija kwa upande wa TANAPAambapoa wanayatumia  kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuvijua vivutio vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini na faida ya kuvitembelea.

 "Ni fursa  ya kipekee  kupitia maonyesho haya kuzitangaza  hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa wakazi wa Tanga lakini pia kwa watanzania wote kuvijua vivutio mbalimbali vilivyopo  kuwafanya kuzielewa hizi mbuga ziko wapi , vivuyio vilivyopo , shughuli zinazofanyika" aliongeza.

 Shirika la hifadhi ya Tanzania 'TANAPA'  linalosimamia hifadhi takribani 22  hapa nchini zikiwemo  Mkomazi, Mikumi , Saadan, hifadhi ya Nyerere, linaendelea kuwakaribisha  watanzania (watalii wa ndani ) kwenda kutembelea na kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana  ambapo oiinhilio ni shilingi elfu tano Mia nne(54000) kwa kila mmoja.

Afisa utalii kutoka bodi ya utalii Tanzania William Halule akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Tanga waliotembelea banda lao latika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako.
 

Afisa utalii kutoka hifadhi za Taifa Tanzania   'TANAPA' Athumani Mbaye akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo jijini Tanga waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya 10 ya biashara yanayoendelea jijini hapa.

Share To:

Post A Comment: