Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya shinyanga Mhe. Johari Samizi amewataka wananchi kutoa taarifa za watu wanaochangia kuhujumu miundombinu katika  miradi mbalimbali ya maendeleo ili serikali iweze kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.

Ameyasema hayo leo Mei 10, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mwamalili katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,ikiwa ni ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo

DC Samizi amewahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika wilaya hiyo ambapo amekumbusha jukumu la kulinda miundombinu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za watu wanaohusika kuharibu miundombinu kwenye miradi ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Aidha Mhe. amizi amewakumbusha wananchi kuendelea kukemea mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana na watoto ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za ukatili wanaofanyiwa wanajamii  hasa wanawake na watoto.

“Ukatili unapotokea tutoe taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa ubakaji, ulawiti vyote hivyo ni vitendo vya ukatili tusivikumbatie kwa kuona kwamba nikisema mwanangu amebakwa au mwanangu amelawitiwa eti unaona aibu sisi wazazi tutekeleze majukumu yetu kwa kuhakikisha kwamba tunawalea na kuwalinda watoto wetu ili kuepukana na mambo yasiyofaa ambayo yanasababisha mmomonyoko wa maadili hata maandiko hayajawahi kusema hivyo tunapaswa tukatae ukatili na aina yoyote ya mmomonyoko wa maadili kwenye maeneo yetu”.amesema DC Samizi

Wakizungumzia suala la Maadili baadhi ya wananchi wamesema ni jukumu la kila mzazi, mlezi na jamii kukemea mmomonyoko wa maadili.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo leo ametembelea na kukagua miradi katika kata ya Mwamalili, Old Shinyanga pamoja na kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Katika ziara yake amefuatana  na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo wananchi wameuliza maswali juu ya jero zao huku viongozi hao wakijibu na kwamba baadhi ya changamoto wameahidi kuzishughulikia kwa uharaka.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza katika kata ya mwamalili ikiwa ni sehemu ya ziara yake leo Mei 10,2023.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza na wananchi katika kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili ikiwa ni sehemu ya ziara yake leo Mei 10,2023 baada ya kutembelea na kukagua hatua mbalimbali zilizofikiwa kwenye Zahanati ya kijiji cha Seseko pamoja na ujenzi wa choo katika shule ya msingi Ujamaa.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: