Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya usanifu wa ujenzi wa mradi wa majitaka katika jiji la Dodoma utakaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA).



Akizungumza baada ya kushuhudia Utiaji saini huo , Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa lengo ni kuendana na ongezeko la kasi la watu katika Jiji la Dodoma na uzalishaji wa 

majitaka ambapo majitaka yasipowekewa utaratibu mzuri huingia katika eneo zima la uchafuzi wa Mazingira.



Mradi huo Wa kuboresha Huduma ya uondoshaji na kutibu Maji Taka Jijini Dodoma ambao utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 5,225,000 sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Bilion 12.3. ambapo 

Mkataba huo umesainiwa kati ya Mamlaka ya Maji safi na usafi Wa mazingira Jijini Dodoma (DUWASA) na Kampuni ya DOHWA Kutoka Nchini Korea ya Kusaini.


"Tunaambiwa kuwa Asilimia 80 ya Majisafi yanayotumika na binadamu katika matumizi yake ya kila siku hugeuka kuwa Majitaka sasa tujiulize yanakwenda wapi zaidi ya kwenda kuchafua Mazingira?,"amesema Aweso



Mhe.Aweso amesema kuwa asilimia ishirini (20) pekee ya wakazi wa Dodoma wanapata huduma ya uondoshaji majitaka katika kata 14 kati ya 41 kupitia mtandao wa DUWASA uliopo, ambao ufanisi Wake hauendani na ongezeko la kasi la watu katika Jiji la Dodoma na uzalishaji wa Majitaka.


Hata hivyo Aweso amekiri kuwa Wizara ya Maji hawajafanya uwekezaji wa kutosha katika eneo la uondoshaji wa Majitaka na kwamba Mazingira ukiyalinda Yatakulinda Bali ukiyaharibu Yatakuadhibu.


Akitoa taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa gharama za mradi huo kwenye Usanifu na Ujenzi unategemea kugharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 70 sawa na Shilingi Bilioni 164.85 za Kitanzania ambapo Mhandisi Aron amesema ,Mkataba wa Usanifu na Usimamizi wa Ujenzi wa Mradi huo utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 5,225,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 12.3.



Mradi huu unalenga kuhusisha Usanifu na ujenzi wa Mabwawa mapya makubwa 16 yenye uwezo wa kutibu takribani lita milioni 20 kwa siku,usanifu na ujenzi wa bomba kubwa (trunk main) kwa kilometer 107.5,ubadilishaji wa bomba chakavu kilomita 2.6 na ukarabati wa Kilomota 2.1 za Mtandao wa majitaka,"amesema Mhandisi Aron



Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha Miezi 49 kutoka tarehe ya leo ambapo awamu ya kwanza Mhandisi Mshauri atafanya kwa muda wa miezi 13 kusanifu Mradi Wa awamu ya pili ambapo atatumia miezi 36 katika ujenzi wa Mradi huo.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: