Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kasulu ameipongeza na kuishukuru benki ya CRDB kwa kuweza kuchangia ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu wanaosoma shule ya msingi kalema.

Aliyasema hayo jana mei 11,2023 wakati akikabidhiwa mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi za kitanzania 1,200,000 kutoka tawi la benki ya CRDB  Kasulu  na kusema"tuliwaomba msaada wa saruji na leo wametimiza kwa kutuletea hii italeta chachu ya maendeleo kwa sekta ya elimu na itawasaidia watoto hawa ambao wanatoka umbali mrefu kuja kusoma na itawaepusha na athari zinazoweza kuwasababisha wasiweze kufika shuleni kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili".

Kwa upande wake meneja wa tawi la CRDB  kasulu bw.Kilian  Ladislaus amesema ,"fedha zilizochangia kununua saruji hizi zinatokana na mapato ya asilimia moja ya wateja wa benki yetu wa hapa kasulu hivyo kufanya kwetu hivi tutakuwa tumechangia uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia watoto wetu hasa hawa wenye mahitaji maalumu".

Share To:

Post A Comment: