Katika kuazimisha siku ya wauguzi duniani leo tarehe 12 mei 2023 wauguzi wote wa halmashauri ya Mji wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ili kuendelea kuweka imani na kuondoa dhana potofu kwa watu wanaowahudumia.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Dr.Erick Mwijage ambaye ni mfamasia wa  mji wa kasulu na kusema,"kumekuwa na dhana potofu za wauguzi japo sio wote kuwaomba kina mama pesa ili wawasaidie wakati wa kujifungua jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa kada yetu ya afya hivyo niwaombe mfanye kazi kwa weledi na nidhamu ili kuweka heshima kwa watu tunaowahudumia kwa kuona watu wa afya ni watu wa upendo na huruma".

Kwa upande wake mmoja wa waaguzi hao bi sifa ezekieli alisema kuwa," maadhimisho haya kwanza yanatuunganisha na kutukutanisha wauguzi ambao tunafanya kazi kwenye vituo mbalimbali vya afya vya hapa mjini kasulu na vinatukumbusha kufanya kazi kwa weledi na hata wale wenye kuteleza katika majukumu yao kurudi katika mstari niwaombe tu jamii wawe na imani na sisi wauguzi ili watupe nafasi ya kuwahudhmia vizuri".

Katika kuhitimisha maadhimisho hayo ya siku ya wauguzi duniani wauguzi hao walifundishana namna ya kumsaidia mtoto kupumua kipindi anapozaliwa ,wakaapa kiapo alichoapa mwazilishi wa wauguzi duniani  mama frolence nightngale na kumalizia kwa kuwatembelea wakina mama wajawazito na waliojifungua na kuwapatia zawadi.

Share To:

Post A Comment: