Mkuu wa Wilaya ya Njombe kissa Kasongwa amewataka wanunuzi wa Parachichi kuzingatia sheria na taratibu ikiwemo kuwa na vibali kutoka serikalini ili kuondoa udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wanunuzi wasio waaminifu.

DC Kissa amesema hayo wakati akifungua mkutano wa wakulima wa Parachichi unaofanyika katika halmashauru ya mji Njombe (Lunyanywi) ambapo amesema lengo la serikali ni kuona mkulima ananufaika na zao la parachichi lakini kama madalali hawatadhibitiwa wataendelea kuwaibia wakulima.

"Kikao hichi kinalenga kusikiliza, kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa parachichi kuanzia kwenye uzalishaji mpaka sokoni"


Kwa upande wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe Emmanuel George amesema parachichi za mkoa wa Njombe zina ubora unaotakiwa lakini lazima kuwe na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha wakulima wanazingatia kanuni za kilimo bora na kuacha tabia ya kuvuna parachichi ambazo hazijakomaa

Share To:

Post A Comment: