Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wilaya ya Arusha Mjini Ndugu Hassan Mndeme leo ameongoza wajumbe wa kamati ya Utekelezaji kufanya ziara ya uimarishaji wa Jumuiya katika kata ya Baraa.


Wakiwa katika kata hiyo walianza kwa kufanya kikao Cha Ndani na viongozi na wanachama wa Jumuiya Baraa na kufuatiwa na kukutana na makundi mengine ambayo yanamfungamano na Jumuiya ya vijana.


Ziara ya Mwenyekiti wa Vijana Ndugu Mndeme pia ilihusisha kutembelea kituo Cha kutolea mafunzo kwa mabinti waliopewa ujauzito katika umri mdogo ili waweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kujitegemea kupitia ujuzi wanaopewa kituoni hapo FARAJA CENTER


Akiwa kituoni hapo Mwenyekiti ameahidi kuendelea kushirikiana na Uongozi wa kituo kwa kuwapeleka wadau Mbalimbali ili kuweza kusaidia katika kukidhi baadhi ya mahitaji ya Msingi kwa kituo hiko.

Aidha Mwenyekiti ametembelea makundi Mbalimbali ya vijana kama bodaboda na wajasiriamali na kuzindua mashina ya wakereketwa katika maeneo Yao.


Imetolewa na

RASULY AWADH BOHA

KHC UVCCM ARUSHA MJINI



Share To:

Post A Comment: