Na;Elizabeth Paulo, Dodoma

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Imedhibiti ndege aina ya kwelea kwelea milioni 227.4 na kufanikiwa kuokoa Tani 1056.3 za mazao ya nafaka.

Udhibiti huo umefanyika katika Mikoa ya Tabora ,Kigoma,Geita, Shinyanga, Mwanza Mbeya , Pwani, Arusha, Manyara na Kilimanjaro kwa kutumia ndege maalumu kutoka shirika la kilimo na chakula duniani (FAO), na ndege nyingine kutoka shirika la Kudhibiti.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru Amebainisha hayo leo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Machi 01, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.

“Hizi tani zilikua ziharibiwe na hawa ndege aina ya kwelea kwelea ndege ilifanya upelelezi wa awali tukaona kwamba kuna haja ya kufanya jitihada za kuokoa mazao hayo ikiwa moja ya majukumu ya mamlaka yetu.”Alisema Ndunguru

Aidha amesema kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kudhibiti nzige wekundu (IRLCO-CSA), Mamlaka imefanya ufuatiliaji kwa njia ya anga kwenye mazalia ya asili ya nzige wekundu kwenye jumla ya hekta 195,150 kwa kutumia helikopta na kubaini hekta 1,000 zilizokuwa na kiwango kikubwa cha nzige.



Prof. Ndunguru amesema Mamlaka inafanya ukaguzi wa mazao yanayotoka na kuingizwa nchini ambapo imekagua tani milioni 5 Laki 3 za mazao ya nafaka, bustani, mizizi, mbegu za mafuta katika vituo vya mipakani,bandari na viwanja vya ndege ambapo Jumla ya vyeti 29,033 vya usafi wa mimea kwa ajili ya kuruhusu mazao kusafirishwa nje ya nchi na vyeti 3359 vya kuruhusu mazao kuingia nchini vimetolewa.

Katika kutatua changamoto za Wakulima kutokua na uelewa wa Matumizi ya Viuatilifu Mamlaka imetoa mafunzo kwa Wakulima, Maafisa Ugani na Wauzaji wa Viuatilifu wapatao 215 kutoka maeneo mbalimbali nchini ili kulinda afya ya walaji, wanyama na mazingira.

Aidha amesema katika Kudhibiti athari za viuatilifu Mamlaka imepima afya za watumiaji wa Viuatilifu 403 kwenye mashamba ya maua Watumiaji 70 sawa na asilimia 17.36% walipatikana na viwango vidogo vya masalia ya viuatilifu hivyo ushauri ulitolewa kwa Wahusika.

Akizungumzia changamoto zinazojitokeza katika utendaji wao wa kazi  Profesa huyo amesema Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wenginej juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na elimu juu ya visumbufu na namna ya Kudhibiti ambapo Mamlaka inaendelea kutoa Mafunzo kwa Wakulima na Wadau wengine 

“Mbali na changamoto hiyo pia  kumekuwepo na wauuzaji wa Viuatilifu namazao ya mimea wasio waaminifu”.



Kadhalika amesema Mamkala itandelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara viuatilifu kwa watengenezaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji ili kupunguza athari ya kuwepo kwa viuatilifu bandia ambapo Katika kipindi hiki, mamlaka inafanya ukaguzi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe, Morogoro, Mbeya.

Kwa upande wake Dkt. Mohammed Hussein Mpina kutoka Idara ya Viuatilifu ametoa wito kwa wale wanaojihusisha na vitendo vya usambazaji wa Viuatilifu bandia nchini kuacha mara moja kwani sheria zipo na hatua zitachukuliwa kwa atakaye bainika na Kufikishwa Mahakamani ambapo amesema kwa uzoefu wa wakaguzi wa mamlaka kuna maeneo ya mpakani mwa nchi jirani zinakua na Viuatilifu bandia na zingine zilizosajiliwa nchi jirani na Huingizwa Tanzania kwa njia isiyo ramsi na kutumika bila kutabuliwa na Malaka.

“Sheria inasema ukikutwa na kosa hili inatosha kabisa kufungiliwa mashitaka na tunazo kesi kadhaa zinazoendelea ambazo kwa namna moja ama nyingine wamejihusisha na upatikanaji wa biashara bandia”.

Amesema mitambo iliyopo ni bora na Imara yenye kutambua Viuatilifu Bandia ambayo inakidhi Matakwa ya kimataifa na?uhitaji wa Soko.




Pamoja na hayo ametaja namba ambazo mkulima anaweza kuzitumia anapohitaji taratibu za huduma pamoja na bei zake 0800110031 na kwa mtu yeyote anayehitaji taarifa za Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu.


Akitolea Ufafanuzi wa umuhimu wa Karantini za wazi Kaimu Mkuu Karantini ya Mimea ya Taifa Dkt Ben Ngowi amesema Karantini hizo ni muhimu kwaajili ya kukagua Mimea au Vipando zinazoingizwa nchini kupitia mipakani zinakaguliwa kabla ya kusambazwa kwa wakulima kutokana na Uwezekano wa kuingiza magonjwa kuliko mbegu halisi.


“Mamlaka ikijiridhisha inavitoa kwenye karantini kwa vibali na kwenda kwa wakulima sasa Karantini zilizopo nchini Tanzania kwasasa hivi maana zingine zinakuja na kuondoka Kushindana na mzunguko wa maisha wa yale mazao na sasa tuna Karantini za mazao manne Zao la Miwa,Vipando vya Miwa Karantini ipo katika kituo cha Tari Kibaha, Shamba la Kilombero, Karantini ya viazi Mviringo Katika mikoa ya Arusha (Arumeru), Niombe, na Mbeya.”Alisema Dkt. Ngowi


Ameendelea Kusema “Kuna Karantini ya Matunda ya Sapodila kule Mkoa wa Manyara wilaya ya Babati hiyo mbegu imekuja kutoka India hatukuruhusu iingie kwa wakulima lakini hatukuikataa bado ipo kwenye majaribio Mamlaka inachunguza uwezekano wa Wadudu waharibifu na magonjwa kama walikuja na hayo mazao/Vipando kutoka nchi ya India. ”Alisema Ngowi


Mamlaka inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Kilimo kwa kuwezesha Mamlaka kufanya kazi zake za kusimamia afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu.


TPHPA imeanza rasmi Julai, 2022 kwa ajili ya kukidhi matakwa ya masoko na mikataba ya kimataifa (IPPC) pamoja na Mazingira salama kwa Afya ya Binadamu, Wanyama na Mimea.

BAADHI YA PICHA ZA MITAMBO BORA KATIKA KUBAINI VIUATILIFU BANDIA.







Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: