Mkuu wa Dawati la Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF-Net) wa Makao Makuu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Eva Stesheni akiwa pamoja askari wa vyeo mbalimbali Februari 28, 2023.


ACP Shetani ametoa elimu ya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya Watoto kwa Wanafunzi wa shule ya msingi Mpunguzi Jijini Dodoma yenye idadi ya Waalimu 16 , Wanawake 12, Wanaume 4 na Wanafunzi 1154 ikiwa ni Mwendelezo wa Kampeni Maaalumu ya Mtandao huo wa Polisi Wanawake kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani.


Aidha amewafundisha wanafunzi mbinu za kujiepusha na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha malengo yao hasa kwa watoto wakike kama vile kupewa lifti, chipsi na zawadi kutoka kwa watu wenye nia ovu.



Pia amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili mema katika Jamii inayowazunguka kama vile kuwaheshimu na kuwatii wazazi, Waalimu pamoja na watu wote mkubwa kwa mtoto, na kuachana na tabia za kupenda kwenda katika mabanda ya video ambayo mara nyingi huonesha picha zisizo na maadili.


Hata hivyo , ACP Stesheni amewataka wanafunzi hao kufichua vitendo vyote vya unyanyasaji watakavyofanyiwa Nyumbani, shuleni na sehemu zozote zile ambazo watanyanyasiwa kwa Wazazi, Waalimu,katika ofisi yoyote ile ya Serikali.


Pia, Mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bw. Busuna Matoja ametoa shukrani za pekee kwa Jeshi la Polisi kwa kufika shuleni hapo na kutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na waalimu waliohudhuria mkutano huo na kusema kuwa kama shule walianzisha Dawati maalumu la kusikiliza na kushughulikia matatizo yote ya Unyanyasaji na Ukatili wanayofanyiwa Wanafunzi wa shule hiyo.



Sambamba na utoaji wa Elimu hiyo Mkuu wa Dawati la Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF-Net) wa Makao Makuu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Eva Stesheni alipata nafasi ya kutoa Burudani ya Wimbo wenye maudhui ya kupinga ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya Watoto pamoja na kupiga picha ya pamoja na waalimu na wanafunzi wa shule ya Mpunguzi.




PICHA NA BENEDICT MLAWA WA JESHI LA POLISI

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: