Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa katika kikao, kilichowakutanisha  viongozi wa Mila (MALAIGWANANI) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa MB, Innocent Bashungwa, Ambapo amemueleza Waziri huyo kuwa Jamii ya kifugaji wa Monduli hawana mgogoro  wowote na Jeshi , huku akiomba kuimarishwa kwa Umoja na ushirikiano ulokuwepo mwanzoni .

" Mh waziri nikushukuru kwa kukubali wito wangu kuja Monduli lakini pamoja na shukurani zote hizo naomba kukuhakikishia kuwa sisi na Jeshi hatuna mgogoro wowote , lakini niseme Moja muhimu Silaha (Risasi) ni kwa ajili ya kulinda mipaka na sio kutoa uhai wetu nikuombe mh waziri ulipokeee hili , ndugu pale Lashaine wapo ambao wameuwawa kwa kutumia silaha tunaomba uangalie hili Lakini pia fidia , FIDIA haiwezi kuwa na Dhamani kwa Mifugo yetu , tuendeleze umoja ulokuwepo kwamba Eneo lile ni la Mazoezi ya Kijeshi lakini pia ni Sehemu ya Malisho" Amesema Fredrick Lowassa mbunge

Fredrick ameongeza kwa kusema kuwa Ulipaji au utoaji ni njia ya kuwafukuza Wafugaji wasiwe na Haki ya kukanyaga eneo Hilo kwa Malisho.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndugu Issack Copriano , Mbali tu na kumshukuru Rais Kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo amesisita pia umoja ulokuwepo Awali kuendelezwa na kusema Fidia si njia ya kutatuta changamoto hiyo Bali ni njia ya Kuwaondoa kuwafukuza wafugaji katika Eneo Hilo.

Awali wakizungumza Baadhi ya Malaigwanani akiwemo Edward Sapunyu, Njokut Alami, na Laigwanani Olengine, kwa pamoja wamesema kimsingi hawana mgogoro wowote na jeshi la Wananchi  juu ya matumizi ya Eneo la kijeshi kwa ajili ya Malisho ya mifugo na kwamba taarifa zinazoenea hazina ukweli wowote, na kuomba kuwepo na Alama ya kimaandishi kama vibao vinavyoonyesha Eneo hili ni la mafunzo ya kijeshi na Malisho.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh Joshua Nassari amewaasa viongozi hao kuwa pamoja na kudai umoja huo na ushirikiano katika eneo Hilo kwa ajili ya Malisho , watumie mifugo hiyo pia kuwapeleka watoto shule kwani Elimu pekee ndiyo uchumi na Maisha ya Sasa.

Baada ya kusikiliza kero hizo , Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Innocent Bashungwa mb, amesema Serikali itaendelea kujenga ustawi wa ushirikiano hayo na kuhakikisha , Jeshi la Wananchi linashikirikiana vyema na wananchi.


Share To:

Post A Comment: