Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange( Mb) amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido kumsimamia Mkandarasi ili kuhakikisha anaondoa milango yote iliyo chini ya viwango na kuweka mirango mingine mipya kwa gharama zake katika Kituo cha afya Ketumbeine wilayani Longido.

Dkt. Dugange ametoa maagizo hayo leo Machi 06, 2023 wakati akikagua ujenzi wa kituo cha afya kitumbeine na kuonesha kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya ambacho tayari kimeaza kutoa huduma.

“Serikali imeelekeza milango yote katika vituo vya kutolea huduma za afya iwe ya Mbao za “Hardwood” lakini vyie mmetumia Mbao mnazozijua wenyewe ambazo ni kinyume na BOQ na maelekezo ya Serikali” amesema Dkt. Dugange.

Dkt. Dugange amesisitiza kuwa, ifikapo tarehe 30 Machi 2023, mzabuni aliyepewa kazi ya kuweka mirango katika majengo hayo awe amebadilisha mirango yote iliyochini ya viwango na kuweka mirango mingine yenye viwango kwa gharama zake mwenyewe.

Kadhalika, Amesema Serikali haitakubali kuingia hasara kwa kulipa fedha mara mbili na haitamfumbia macho mtumishi yoyote anayeshindwa kutimiza wajibu wake kwa kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo.

Sambamba na hayo, Dkt. Dugange ameelekeza ujenzi wa majengo ya awamu ya pili ambayo ni Jengo la x- ray, Jengo la kufulia na nyumba ya watumishi (2 in 1) yawe yamekamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo tarere 30 Machi 2023.

Vile vile, ameagiza ifikapo tarehe 1 Mei 2023 majengo ya awamu ya tatu ambayo ujenzi wa jengo la Wagojwa wa ndani na nyumba ya Watumishi (3 in 1) yawe yamekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.



Share To:

Post A Comment: