Na Denis Chambi, Tanga.
TAASISI ya Masjid Muzdalfa kwa kushirikiana na Waterfall Charity UK kutoka nchini Uingereza imekabidhi Nyumba 6 kwa familia za watoto yatima wilayani Tanga hii ikilenga kuwaondoa katika Mazingira magumu.
Taasisi hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi wake Al Haji Twaha Omari Tawakal ambayo inamiliki shule ya msingi ya Muzdalfa Mwakidila ikishirikiana na waterfall Charity UK inawalipia ada wanafunzi yatima na wasiojiweza 170 shilingi laki nne (400, 000 ) kila mmoja kwa mwaka pamoja na kuwawezesha mahitaji muhimu ya binadamu ikiwemo chakula na maradhi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba hizo katibu tawala msaidizi wilaya ya Tanga Mussa Machunda kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo amewapongeza Muzdalfa pamoja na Waterrfall charity kwa kuyatazama makundi hayo muhimu wakiunga mkono jitihada za kusogeza karibu na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.
"Niwapongeze sana kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya, tunafahamu kuwa kazi ya kutoa huduma kwa jamii ikiwemo elimu, maji, afya na nyinginezo ni kazi ya serikali lakini nyinyi kama wadau mmeamua kuyasaidia kwenye maeneo kama hayo, kwani tunaona tatizo hili la watoto yatima katika jamii sasa hivi limefanya baadhi ya watoto wengi kukosa wazazi hivyo kumfanya mtoto aishi kwenye mazingira magumu na baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kukidhi mahitaji kwa kweli hili ni jambo la kipekee na la kupongezwa"
"Katika mambo ambayo yanakubaliwa na Mungu ni ibada za kuhudumia watu wasiojiweza wakiwemo yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, na ninyi mmeona hiyo ni fursa mkaamua kuwasaidia wayoto wetu na pengine watoto hawa huduma hizi wasingezipata lakini na sisi wengine tupate fundisho kutoka kwa hawa wenzetu tunapojaaliwa kuwa na uwezo wa mali basi tuwakumbuke na wenzetu wahitaji " alisema Machunda
Akitoa taarifa ya Masjid Muzdalfa Fatuma Mgunya amesema kuwa kwa kushirikiana na Water fall Charity wamefanikiwa kuchimba visima vya maji zaidi ya 20 kwajili ya kuwasaidia wakazi wa maeneo mbalimbali kupata huduma ya maji huku wakitoa kiasi cha shilingi Million 40 kwajili ya kuziwezesha familia zenye watoto yatima kujikimu kimaisha.
"Muzdalfa hutoa maji bure kwa wakazi wanaozunguka shule lakini pia kwa kushirikiana na Wayerfall Charity tumechimba visima zaidi ya 20 lakini pia tumeweza kutoa gedha taslimu kwa hawa yatima kwaajili ya kujikimu ambazo mpaka sasa wameshagawiwa zaidi ya shilingi Million arobaini.
Pamoja na hayo taasisi hiyo ya Muzdalfa kwa kushirikiana na Water fall Charity imeweza kuwalipia ada wanafunzi 16 kati ya 36 waliofanya vizuri mitihani yao ya darasa la saba ambao wamejiunga kwenye shule mbalimbali za sekondari katika muhula wa masomo wa mwaka 20223.
Mwenyekiti wa wafadhili mkoa wa Tanga ambaye pia mwenyekiti wa taasisi ya " Wapenda Kheri Foundation" Ally Masomaso amewapongeza na kuwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo water fall Charity ambao wanashirikiana nao katika kusaidia jamii pamoja na mswala ya dini ikiwemo kujenga misikiti huku akizitaka taasisi zilizopo ndani ya Mkoa wa Tanga kuunganaa katika kuziwezesha jamii katika nyanja mbali mbali.
Aliongeza kuwa taasisi ya Kheri Foundation ambayo inaunga mkono katika kusaidia jamii za wahitaji katika nyanya mbalumbali tayari imeshajenga nyumba nne kwaajili ya watoto yatima ndani wilaya ya Pangani pamoja na Misikiti ambapo bado wanaendeleza jitihada hizo.
"Tunawashukuru sana wafadhili wetu kutika nchi tofauti tofauti duniani wamekuwa wakitusaidia katika mambo mbalimbali ya kusaidia jamii pamoja na kujenga misikiti, taasisi ya Muzdalfa tunawashukuru sana kwa msaada huu wanajitahidi sana kwaajili ya kuwasaidia mayatima tukipata taasisi kama hizi na tukaungana iyakuwa ni jambo jema nia yetu sisi ni kuijenga Tanga iwe moja" alisema.
Baadhi ya wazazi na walezi walikabidhiwa nyumba hizo akiwemo Halima Cheo na Fatuma Ally wameishuku taasisi ya Muzdalfa pamoja na Waterfall Charity UK kwa kuwawezesha makazi hayo ambapo awali wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali ya maradhi.
"Namshukuru sana kwa kunipatia hifadhi kama hii kwa kweli sikutegemea Mungu mwenyewe ndiye atakayewalipa sina cha kuwalipa nitaishi na familia yangu , nashukuru uongozi wete wa Muzdalfa na Water fall Charity kwa kutufanyia wema huu" walisema
Post A Comment: