Na Joel Maduka

Watu saba wamefariki dunia huku  wengine  wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria kampuni ya Sheraton lenye namba za usajili T922 ADC iliyokuwa ikitokea Jijini Mwanza kuelekea Lunzewe Wilaya ya Bukombe ajali ambayo imetokea  iliyotokea  kwenye mtaa wa Mwilima kata ya  Kanyara mkoani Geita.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema, ajali imetokea leo Machi 7, 2023 majira ya saa 10:30 jioni na kueleza chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya basi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Martine Shigela amefika kwenye Hospital ya Rufaa Mkoani humo kwa lengo la kuwajulia hali majeruhi ambapo ameagiza kwa Jeshi la Polisi ni vyema likafanya ukaguzi wa mara kwa mara pindi Magari ya abiria yanapotokea Pointi A kwenda Pointi B.

 Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita ambapo majeruhi walipelekwa katika kituo cha Afya Kasamwa kwa huduma ya kwanza na kisha hospitali ya rufaa ya mkoa kwa matibabu zaidi.


Share To:

Post A Comment: