Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange( Mb) ameagiza ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Longido kukamilika kwa wakati ili kuweesha huduma zote za ngazi ya hospitali kuanza kutolewa.

Dkt. Dugange ametoa maagizo hayo Machi 06, 2023 wakati akikagua ujenzi wa Majengo ya hospitali hiyo unaoendelea katika awamu tofauti.

Dkt. Dugange ameridhishwa na viwango na kasi ya ujenzi wa majengo manne amabayo ni Jengo la Upasuaji, Jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wanaume na wanawake ambayo yanatarajiwa kukamilia tarehe 03 Aprili 2023.

Dkt. Dugange ameagiza kuanza kufungwa kwa vifaa tiba ambavyo vimeletwa katika hospital katika baadhi ya Majengo yaliyokamili ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.



Share To:

Post A Comment: