Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa akiongea na vijana waliohitimu mafunzo katika kikosi cha 841 JKT juu ya umuhimu wa kulinda amani ya Taifa la Tanzania.
Baadhi ya vijana waliohitimu Mafunzo katika kikosi cha 841 JKT Mafinga wakionyesha ukakamavu baada ya kuhitimu mafunzo.
Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo katika kikosi cha 841 JKT Mafinga wakionyesha ukakamavu baada ya kuhitimu mafunzo.

Na Fredy Mgunda, Iringa.


WAHITIMU wa mafunzo ya ya awali ya Jeshi la kujenga taifa katika kikosi cha 841 JKT Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa kujijengea uwezo wa kujilinda na kupingana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kujikinga na maambukizi ya VVU.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya awali ya kujitolea kwa vijana wa JKT Oparesheni Venance Mabeyo Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa kutokana na kiapo walichokiapa wanapaswa kuwa waaminifu kwa viongozi na kuilinda nchi.


Salekwa alisema kuwa mafunzo hayo yakawe chachu ya kupambana na kupunguza matukio ya ukatili ambayo yamekuwa yakifanyika katika jamii pamoja na kuishauri jamii kuondokana na mila na desturi zisizo za kiafrika ambazo zimekuwa zikisababisha kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili .

“nina imani kwamba mtakuwa chachu katika kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao umekithiri katika jamii zetu ninyi ni vijana mmepata mafunzo haya naamini mkiamua kwa dhati mnaweza  kubadilisha kabisa taswira ya nchi yetu" Dkt. Salekwa

Kwa upande wake Mkuu wa utumishi Jeshini Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli amewataka vijana hao kutumia mafunzo ya stadi za kazi waliyoyapata na kujiandaa vizuri katika mafunzo ya awamu ya pili ili kuyaendeleza maisha yao hata kama hawataajiriwa .

“concentration ya yale mafunzo mtakayopewa hayatakuwa yanakuingia kwa sababu unawaza kitu kingine tutoe hayo mawazo  tukasikilize yale tunayofundishwa na hata kama utapata mafunzo sehemu nyingine lakini kuna hasara gani kama wewe ulizingatia ufugaji bora wa mifugo na utakapopata hiyo ajira ukawa na sehemu gani ukifuga hiyo mifugo na kukuletea pato la ziada? utakuwa umepata hasara gani utakuwa na dhambi gani nawasisitiza sana sehemu ya pili tunayokwenda tukaiweke kichwani kwetu tuipe nafasi mioyoni mwetu tuip nafasi kwenye ubongo wetu ili tuweze kutimiza lengo zima la jeshi la JKT"

Meja Jenerali Paul Kisesa alisema kuwa mafunzo hayo yakathibitishie uwezo wa vijana wa kitanzania kwa serikali chini ya  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa vijana wanaweza kwa kila jambo na hasa wakiamua .

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Projest Rutaihwa  alisema kuwa vijana wa JKT wanapaswa kuzingatia utunzaji wa afya zao pamoja na kujiepusha na ulevi na tabia zisizokubalika katika jamii .

“pamoja na mafunzo mliyopata mzingatie kiapo chenu zingatie utunzaji wa afya zenu kwani afya ndiyo mtaji katika utendaji wa kazi za kila siku niwasihi jiepusheni na matumizi ya dawa za kulevya ,ulevi na tabia nyingine zisizokubalika katika jamii “

Jesca Mapunda ni service girl na Asery Mbonea ni service man wameahidi kuwa waadilifu na kusimamia mafunzo waliyopata na hivyo kuleta tija katika jamii na matokeo chanya juu ya mafunzo ya stadi za maisha walizopatiwa .

Mafunzo hayo ya awali yamehitimishwa tarehe 07/03/2023 toka yalipo funguliwa tarehe 28 novemba mafunzo yaliyotolewa kwa vijana zaidi ya 400 chini ya mkuu wa kikosi cha 841 JKT Kanali Issa Chalamila  ambayo yana lengo la kuwasaidia  vijana kujitegemea na kulitegemeza taifa .


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: