Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo  amekutana na Bilionea Laizer katika mkutano wa shina namba 26 tawi la Naisinyai Wilayani Simanjiro.

Bilionea Laizer ni moja ya wanachama wa CCM katika shina na tawi hilo, ambalo Katibu Mkuu Ndg. Chongolo leo tarehe 08 machi, 2023 ameshiriki, amesikiliza na kutatua kero za wananchi wa eneo hilo kwa kutoa maelezo mbalimbali kwa serikali katika masuala ya barabara, maji na mengineyo.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Manyara kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani, kuimarisha uhai wa chama pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo ameambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Sofia Mjema pamoja na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.

Share To:

Post A Comment: