👉Amwapisha Mabula Nyanda kuwa Kamisha mpya TAWA

Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza watendaji wa wizara yake kwenda kumaliza migogoro yote baina ya Hifadhi na wananchi kote nchini ikiwa ni pamoja na maelekezo yote aliyoyatoa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi mkoani Manyara hivi karibuni.

Mhe Mchengerwa ametoa maelekezo haya leo wakati akimemvisha cheo Mabula Nyanda kuwa Kamisha mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) na kumuapisha eneo la Kilwa Kisiwani.

Mhe. Mchengerwa amesema migogoro yote inatakiwa kuisha ndani ya miezi miwili ili kazi ya uhifadhi wa raslimali za taifa iweze kutimia na kutimiza ndoto ya mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzani ya kutaka raslimali ziwanufaishe wananchi wa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Aidha amesema kila mtanzania anatakiwa kuheshimu sheria za nchi za uhifadhi wa raslimali ili kutatua migogoro isiyo ya lazima.

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na eneo la zaidi ya 30 ambalo limehifadhiwa kisheria ambapo amesema katika kipindi hiki watendaji wakibaini kuwa kuna sheria ambazo zinaleta changamoto ni vema waziainishe ili zirekebishwe.

Amefafanua kuwa maeneo yanayosimamiwa n TAWA yatakuwa endelevu iwapo watendaji wa TAWA watashirikiana na wananchi kikamilifu.

Pia ameitaka Bodi ya TAWA kwa kushiy na Menejimenti yake kujenga hoja ili visiwa vingine pia visimamiwe na TAWA na kuweka mipango mahususi ya kuvutia wawekezaji makini waje kuwekeza.

Ametoa onyo kali kwa baadhi watendaji wanaokula rushwa na kuingiza mifugo kwenye mapori ya Serikali yaliyohifadhiwa
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: