Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Waziri wa Madini Dk.Doto Biteko amemtaka Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Kheri Mahimbali kutambua thamani ya watumishi kwani muda mwingi wanautumia wakiwa kazini na kwamba nyumbani wanatumia saa tatu huku wakisinzia hivyo wanapaswa kuonwa wao ni watu muhimu katika Wizara hiyo.


Dkt. Biteko amesema watumishi ni watu muhimu kwa kuwa wanatumia muda wa saa nane kazini tofauti na muda wanaotumia wakiwa nyumbani.



Waziri Dkt. Biteko ameyasema hayo jijini Dodoma leo Machi 10,2023 katika kikao cha kumtambulisha Katibu huyo kwa watumishi wa Idara zote zilizopo sekta ya madini na kueleza lengo ni kusimamia malengo waliyowekwa na serikali.



Pia Waziri Dk Biteko amempongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaongezea timu ya wachapakazi katika Wizara hiyo.


"Wafanyakazi hawa hakikisha wanajiona wao ni watu muhimu na wapo wa kila aina na tabia zote unazozifahamu hapa duniani hivyo unapaswa kuwaelewa vizuri. Tuna malengo ambayo tumepewa na nchi tuyasukume yaende salama,"alisema Dkt. Biteko.



Amesema katika wizara hiyo wapo watu wa aina mbalimbali ambao katibu mkuu atakwenda kufanya nao kazi hivyo anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali.


"Ndugu katibu mkuu hapa unaowaona wapo watu wa kila aina wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia dead line hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamazili kwa wakati na wala majibu hawakupi.


"lakini pia wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wafurahi kurekebishwa lakini wengine ukiwarekebisha wanakukasirikia"amesema Biteko



Naibu waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa, amesema yapo mambo mengi ambayo wameyafanyia kazi hadi sasa ikiwemo kupunguza idai ya watu waliokuwa wamekaimu katika nafasi mbalimbali.





"Katibu mkuu nashukuru kuwa umeeleza kuwa unapaenda kufanya kazi kama timu mie pia ni muumini wa ushirikiswaji lakini toka nimeingia madarakani katika nafasi hii mambo mengi tumeyafanyia kazi ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokua wakikaimu katika nafasi mbalimbali.


"Hivyo tunakuomba katika nafasi ambazo bado hazijafanyiwa kazi uone ni namna gani zinafanyiwa kazi ili maeneo yanayokaimiwa yapate watu na kazi ziendelee kwa malengo tuliyojiwekea"amesema Dk. Kiruswa


Awali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Msafiri Mbibo amesema kuwa sekta ya madini ni muhimu katika uchumi, maisha na maendeleo kiujumla na kwamba rasilimali za madini zilihifadhiwa na waasisi wa nchi hivyo wataendelea kuzisimamia kwa maslahi ya Watanzania.


"Tumepewa dhamana ya kuzisimamia na kufanya utekelezaji mzuri na wenye tija kwa maslahi mapana na nchi yetu, tuna vitu vitatu ambavyo tunatakiwa kuviangalia kama Wizara vikiwamo uadilifu ,uwahibikaji na njonzi pana ambazo ni za kuzisimamia rasilimali za madini," amesema Mbibo

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: