Na Denis Chambi, Tanga.

Uongozi wa  Seneti ya vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Tanga umemshukuru na kumpongeza  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa hatua aliyoichukuwa ya kuongeza  kiwango cha fedha za kujikimu (Boom) kwa wanafunzi wa elimu ya juu waliopo katika vyuo nchini mbalimbali hapa nchini kutoka kiasi cha shilingi  elfu nane mia tano  (8500 ) hadi  elfu kumi (10, 000) kwa siku jambo ambalo limewapa faraja na ari katika masomo yao.

Pongezi hizo zinakuja kufwatia mkutano uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni wa Rais Dkt Samia  Suluhu Hassan kukitana pamoja na   viongozi wa shirikisho la vyuo vya elimu ya juu Tanzania bara  'TAHLISO' pamoja na wale wanaowakilisha visiwani Zanzibar  'ZAHLIFE'  ambapo rais alitangaza neema hiyo  iliyopokelewa kwa furaha na wanafunzi hao.

Akizungumza mwenyekiti wa Seneti mkoa wa Tanga Hamilton  Ezekiel alimpongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hatua hiyo  sambamba na kuwapatia ofisi ya samani kwaajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za umoja huo.

"Kwa heshima na taadhima nachukuwa fursa hii kumshukuru sana Rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake wa dhati kwa kukubali kuzungumza na sisi vijana wa vyyo na vyuo vikuu,  shabaha ya Rais imeonekana kwetu,  kwa niaba  ya vijana wa Seneti mkoa wa Tanga ninabeba  ajenda kwa kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali ya Rais na nitaendelea kuwa mkarimani wa vijana wenzangu kwa yale yote yatakayofanywa na yaliyofanywa  na serikali inayoongozwa na  Mheshimiwa Rais  Dkt Samia Suluhu Hasaan,  hakika ilikuwa ni siku ya kipekee na ni ya  historia kubwa kwetu tuna deni kubwa kwake " alisema Ezekiel.

"Kwa niaba ya vijana wa Seneti mkoa wa Tanga tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuweza kupandisha kiwango cha fedha ya kujikimu (Boom) kutoka shilingi elfu nane na mia tano hadi elfu kumi kwa siku asante sana Rais wetu,  sisi kama vijana  tuna deni kubwa sana la kwenda kuyasema mema yote na kazi kubwa unayoifanya katika nchi yetu ya Tanzania"

Pamoja na pongezi mwenyekiti huyo ameiomba serikali kwa kupitia  bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 kungalia namna ya kuwasaidia fedha za kujikimu wanafunzi waliopo vyuooni  katika ngazi ya cheti na astashahada ombi ambalo pia lilipokelewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Share To:

Post A Comment: