Kaimu meneja wa elimu na huduma  kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania Stephen Kauzeni akizungumza mkoani Tanga katika semina kwa  wanachama wa miliki wa mabasi Tanzania  
Mwenyekiti wa wamiliki wa mabasi na wasafirishaji mkoa wa Tanga 'TABOA' Abdi Awadhi akizungumza  kwenye semina iliyotolewa na mamlaka ya mapato Tanzania kuhusu huduma hiyo wanayoitoa hapa nchini .
Meneja wa  Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Tanga akifungua semina iliyotolewa kwa wamiliki wa mabasi na wasafirishaji mkoa wa Tanga 'TABOA.
Baadhi ya wanachama wamiliki wa wa mabasi Tanzania 'TABOA' mkoa wa Tanga wakifwatilia semina iliyotolewa leo mamlaka ya mapato Tanzania kuhusu huduma ya usafirishaji pamoja na mabadiliko ya sheria ya usafirishaji nchini.
Na Denis Chambi, Tanga.

MAMLAKA  ya Mapato Tanzani 'TRA' imewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi yanayoenda masafa marefu hapa nchini kuendelea  kutumia mfumo wa tiketi mtandao kulingana na sheria ya usafirishaji iliyowekwa sambamba na kulipa kodi kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa na kaimu meneja wa elimu na huduma  kwa mlipa kodi Stephen Kauzeni mkoani Tanga wakati wa  semina  kwa wanachama wamiliki wa mabasi Tanzania 'TABOA' ambapo amesema kuwa mfumo huo ambao umeshaanza kutumika kwa baadhi ya maeneo hali ambayo pia itaweza kuchangia pato la Taifa huku ukisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza udanganyifu uliokuwa ukifanyika.

"Ushiriki umekuwa mzuri katika mfumo huu mategemeo yetu ni kwamba watu wengi ambao wameendelea kujiunga na huu mfumo na wameanza kuelewa kwa sababu hii itaipa nafasi serikali kupata mapato kwaajili ya malengo mbalimbali pia itawasaidia walipa kodi kuweza kujua kabisa  kiwango cha pesa ambacho wanakipata lakini pia wizi mdogo mdogo umeondoka baada ya kutumia tiketi mtandao" alisema Kauzeni.

Aidha wamiliki wa vyombo vya usafiri yakiwemo magari ya abiria yanayoenda masafa marefu wametakiwa kulipa kodi kwa wakati ili kuepukana ma changamoto mbalimbali ikiwemo kusitishiwa huduma zao hapa nchini huku wakotakiwa kuendelea kuweka kumbukumbu zao kilingana na walivyoelekezwa kisheria.


Akizungumza kwa niaba ya Wanachama wamiliki wa mabasi Tanzania 'TABOA' mwenyekiti wa umoja huo  mkoa wa Tanga na wasafirishaji  Tanzania Abdi Awadhi ameeleza changamoto wanayokutana nayo ha  kokosekana kwa mtandoa kwa baadhi ya maeneo wanapokuwa njiani wakati wa safari zao  hali ambayo imekuwa ikiwafanya kushindwa kutoa tiketi mtandao kwa abiria kama ilivyoelekezwa na serikali.

"Changamoto kwenye sekta ya usafirishaji kwa mabasi zipo nyingi ikiwemo mitandao mingi kupote potea hovyo tunapokuwa njiani tiketi zinaharibika na hata zile karatasi tunazotumia  kukatia tiketi zinakuwa hafifu tunapata gharama kubwa  ya ziada ma sisi tumekubali kwa moyo mmoja kutumia tiketi mtandao baadhi ya mabasi yameshaanza na tunaendelea"

"Tumeletewa sera mpya ya mapayo ambayo tunatakiwa msafirishaji alipe  laki tano kwa mwaka bila kueleza n basi ya aina gani kuna basi nyingine ni chakavu na mpya tungeomba mamlaka ya mapayo ilione hilo kupunguza kodi waliyotuwekea na watoze kodi kulingana na umri wa mabasi " alisema Abdi.

Aidha Kupanda  cha  bei ya mafuta hapa nchini kwa vyombo vya usafiri ikiwemo diesel na Petrol  kumewaibua wamiliki hao kuwa kama changamoto kwao licha ya kuwa bado kiwango cha nauli wanazotoza kwa  abiria ni ndogo  hali ambayo inawafanya kulipa kodi wanzotakiwa .

Akizungumza meneja wa Tiketi mtanao kutoka mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini 'LATRA' Thadei Mwita amesema mfumo huo umesaida kwa kiasi kikubwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuju kiasi cha  fedha alichokusanya kwa wakati huku ukiisaidia serikali kuweza kumwekea makadiria ya kodi ambayoa anatakiwa kulipa kwa mwezi.

Aliongeza kuwa kumekuwa na ushindani wa kibiashara  kwa wamiliki wa mabasi wengi wakifanya safari zao bila kuwa na abiria wa kutosha jambo ambalo limekuwa likiwaathiri kwa kuingia gharama ambazo zimekuwa ni maumivu kwao.

"Kuna tatizo kubwa ambalo ni sugu la ushindani hasi wasafirishaji wanashindana bila tija wanatoa mabasi mengi kwa wakati mmoja na wakati mwingiene yote yanaenda yakiwa na abiria pungufu maana yake hasara inakuwa ni kubwa kwasababu kipato wanachopata hakiendani na gharama ya mafuta na gharama nyinginezo"

Alisema kuwa kwa  kupitia mfumo huo wa Tiketi mtandao  umewasaidia kwa kiasi kikubwa wamiliki wa mabasi na kuzuia mianya ya upotevu wa mapato pamoja na fedha ambazo walipaswa kupta lakin awali zimekuwa zikienda moja kwa moja kwa wapiga debe huku akiwataka  wamiliki wa vyombo vya usafiri kujiunga katika umoja ili kupata sehemu ambayo wanaweza kupata msaada kwa wakati.

Share To:

Post A Comment: