Na Woinde Shizza , ARUSHA 

Bodi ya sukari (SBT )inashirikiana na wadau wa maendeleo  wakiwemo taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo (TEMDO) ilikuboresha  kuboresha na  kubuni mitambo ya kisasa ya kuzalisha sukari kwa wingi itakayowezesha wakulima na wafanyabiashara  kuanzisha viwanda vya kuzalisha sukari hapa nchini.

Sekta ya viwanda nchini  ni kiungo  muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa taifa  hali ambayo iliopelekea naibu waziri wa Kilimo Antoni Mavunde  kufanya ziara  katika taasisi ya ubunifu  na usanifu mitambo (TEMDO)na kuona ubunifu wa mitambo ya kilimo itakayokuza biashara ya sukari hapa nchini.

Akiongea katika ziara hiyo Naibu waziri huyo alisema kuwa  ni lazima  tutengeneze mashine au viwanda  ambavyo vitasaidia wakulima   kuongeza dhamani katika mazao yao

"Lazima tufikie katika kuongeza dhamani na nyinyi mliopo  chini ya wizara  ya viwanda , biashara na uwekezaji muakikishe mnafanya kazi ya kutengeneza  mitambo ya kuongeza dhamani na hasa katika mazao ya kilimo ,uvuvi pamoja na mifugo mmepewa jukumu kubwa  kama temdo na  mimi ningependa kila siku muendelee kuja na bunifu mbalimbali  " alisema 

Alisema kuwa wanaamini mitambo hii  ikikamilika  kwa muda muaafaka kama walivyomuaidi hadi kufika   mwezi June  itasaidia kumtoa mkulima katika ukulima   wa miwa  na kwenda kuwa mzalishaji  wa sukari.

"Niwaombe muendelee kuboresha huduma mnayo nafasi kubwa ya kuwasaidia wananchi ,pia nimpongeze mkurugenzi wa bodi ya sukari  Kwa bunifu walioufanya na kuamua kushiriana na TEMDO  mlikaa na  kutafuta jinsi ya kumsaidia mkulima kuondoka  na tatizo la miwa kubaki shambani  na kuharibuka ,kuna kipindi uwezo wa uchakataji wa miwa katika viwanda vikubwa uliwaliwazidi nakuanza kutokuchukuwa miwa ya wakulima ,bodi iliamua kuchukuwa hatua kwamba huyu mkulima aliekwenda shambani akaweka mda wake akatumia gharama leo miwa yake inaozea shambani hali ambayo ilikuwa inawavunja moyo wakulima ,lakini pia kama nchi tulikuwa tunajipunguzia mapato  lakini pia tulikuwa tunawafanya watu wachukie kilimo   hivyo  Mtambo wa Kuzalisha Sukari  utamuokoa mkulima .

Alibainisha kuwa mtambo huu  utasaidia kuongeza dhamani ya mazao ya kilimo kwa yule mkulima ambaye analima miwa na yupo sehemu ambayo awezi kupeleka miwa yake katika kiwanda kikubwa  na utasaidia kukuza uchumi wetu  wa nchi yetu ,na alisisitiza kuwa lazima taasisi hizo zijikite katika kutengeneza mitambo itakayo saidia  kuongeza thamani katika mazao  ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof.Keneth Bengesi alisema kuwa   lengo la kutengeneza mashine hii ni kuhakikisha wanamsaidia mkulima pamoja na kuhakikisha kwamba hawauzi mazao ya miwa ambayo hayajaongezewa dhamani  maana mkulima anapoongeza thamani mazao yake anapata pesa nyingi zaidi .

Mkurugenzi  wa taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO) Muhandisi  Prof. Frederick Kahimba  alisema kuwa    wameshaanza kutengeneza mitambo mbalimbali itakayomsaidia mwananchi na kuhakikisha yale matatizo ambayo yapo katika wizara ya kilimo wao kama Taasisi ya usanifu wanayatatua na kufanyia kazi.

Share To:

Post A Comment: